Nchini Bangladeshi, inakadiriwa kuwa takribani watu 66,000 wanaishi na uziwikutoona.*
*Shirikisho la uziwikutoona Duniani, 2018 Katika hatari ya kutengwa kwenye utekelezaji wa CRPD na SDGs: Kutokuwepo kwa usawa kwa watu wenye uziwikutoona.
Nchini Bangladeshi, watu walio na uziwikutoona wanachukuliwa kuwa moja ya vikundi vilivyotengwa na vilivyo hatarini zaidi.
Ulemavu wa uziwikutoona kama ulemavu kwa haki yake wenyewe, umetambuliwa tangu mwaka 2013 nchini Bangladeshi. Kabla ya mwaka 2013, watu wenye uziwikutoona walitambuliwa kama watu wenye Ulemavu changamani na ilibidi watafute usaidizi kutoka kwenye vituo ambayo vinatoa huduma kwa watu wenye ulemavu wa kuona na kusikia.
Mnamo mwaka 2013, serikali ya Bangladeshi ilipitisha Sheria ya Haki na Ulinzi wa Watu Wenye Ulemavu (RPPDA) ambapo uziwikutoona umetambuliwa kama aina tofauti ya ulemavu. Kwa jumla, sheria inatambua aina 12 za ulemavu na uziwikutoona ni miongoni mwa aina hizo.
Sheria ya Haki na Ulinzi wa Watu Wenye Ulemavu ni pamoja na haki za jumla kama vile haki ya kuwa hai na kuendelezwa kikamilifu, usawa wa kutambuliwa kisheria na haki, haki za urithi, uhuru wa kujieleza, kutoa maoni na kupata taarifa, haki ya kuishi na familia na kujenga familia na haki ya kushiriki kamilifu katika jamii.
Kundi lingine ni haki za kimsingi ambazo ni pamoja na: upatikanaji, kupata elimu katika ngazi zote za elimu, ajira ndani ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali, kupata fidia ya ulemavu wakati wa ajira, kupata huduma za afya, kupata huduma za kisheria.
Ingawa uelewa kuhusu sheria bado hautoshi, umewawezesha watu kujua zaidi kuhusu haki zao na ni msaada gani wanaweza kupokea.
Ufikiaji wa teknolojia unaweza kuwa chanzo cha mabadiliko kwa watu wenye ,uziwikutoona kutoa njia mpya za kupata habari, kuwasiliana na watu wengine, na kushiriki kikamilifu katika maisha ya kila siku.
Raslimali hizi zitawawezesha watu wenye uziwikutoona na wale wanaowasaidia kuishi, kujifunza, na kustawi.