Ilani hii imesasishwa mara ya mwisho Februari 2024

Tunachukua faragha yako kwa uzito sana na tutajitahidi kadri tuwezavyo kulinda taarifa zako binafsi. Ilani hii ya faragha inaelezea jinsi tunavyokusanya, kuhifadhi na kutumia data zako binafsi pale unapojihusisha na Kitovu cha kimataifa cha rasilimali za Uziwikutoona(deafblindness.info). Pia inaeleza jinsi tutakavyozihifadhi data zako kwa usalama na jinsi unavyoweza kuendelea kudhibiti matumizi yake.

Tunatambua kwamba hapa kuna taarifa nyingi, lakini tunataka upate taarifa iliyo kamili.

Kuwa na uhakika kwamba hatuuzi au kushirikisha taarifa zako binafsi kwenye mashirika mengine kwa madhumuni ya wao kujitangaza.

Iwapo ungependa kupokea ilani hii ya Faragha katika muundo tofauti, (Kusoma kwa urahisi, sauti, chapisho kubwa au Breli) tafadhali wasiliana na Timu yetu ya huduma za wasaidizi:

  • Barua pepe:[email protected]
  • Chapisho: Timu ya Huduma za Wasaidizi, Sense, 101 Barabara ya Pentonville, London, N1 9LG, Uingereza

Yaliyomo

  • Sisi ni nani
  • Ni taarifa binafsi zipi tunazokusanya
  • Unapotumia tovuti yetu
  • Tunachofanya na taarifa yako
  • Kushirikisha taarifa zako
  • Msingi wetu wa kisheria kwa ajili ya kuchakata data zako
  • Jinsi tunavyotunza data zako
  • Muda gani tunahifadhi data zako
  • Haki zako
  • Jinsi ya kuwasiliana nasi
  • Usasishaji wa sera za faragha

Sisi ni nani

Kitovu cha kimataifa cha Raslimali za Uziwikutoona kimeundwa na Sense International.

Sense International ni shirika la hisani linaloongoza kwa kutoa misaada ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wa Uziwikutoona katika nchi za Bangladesh, India, Nepal, Kenya, Peru, Romania, Tanzania na Uganda. Sisi ni shirika la hisani lililosajiliwa nchini Uingereza na Wales (1076497) na kampuni yenye dhamana ya ukomo (03742986).

Kazi yetu inalenga katika kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wa uziwikutoona wanaweza kupata elimu, huduma za afya na njia za kujipatia riziki, ili waweze kustawi na kuishi maisha kwa uwezo wao kamili. Tunategemea ukarimu wa washirika wetu katika kutusaidia kufanya maendeleo ili kuweza kufikia maono yetu ulimwenguni ambapo watu wote walio na Uziwiupofu wanaweza kuwa wanajamii walio sawa na hai ndani ya jamii.

Sense International ni sehemu ya familia ya Sense “familia”. Sense ni shirika la hisani linaloongoza kwa kutoa msaada ambalo limesajiliwa nchini Uingereza na Wales (289868) na ni kampuni yenye dhamana ya ukomo (01825301). Jina lake rasmi ni Sense, The National Deafblind and Rubella Association. Katika hii ilani ya Faragha, maneno ‘Sense’ au ‘sisi’ ‘sisi’ na ‘yetu’ yanaweza kurejelea Sense International au Sense.

Anwani yetu iliyosajiliwa ni 101 Pentonville Road, London, N1 9LG, Uingereza. Tunachangia anuani hii na Sense. Sense ina ofisi, huduma na maduka katika maeneo yote ya Uingereza, Ireland ya Kaskazini na Wales.

Ni taarifa binafisi zipi tunazokusanya

Kwanza, jambo la kwanza ambalo tungependa ufahamu ni kuhusu data binafsi zipi ambazo tunakusanya kupitia Kitovu cha kimataifa cha Raslimali za uziwikutoona duniani, na jinsi tunavyozikusanya.

Taarifa unazotupa

Haya ni maelezo kuhusu wewe ambayo umetupatia kwa kutuandikia barua, simu, barua pepe au vinginevyo. Inajumuisha maelezo unayotoa unapouliza, kutoa mrejesho kuhusu raslimali, au kutumia vipengele vingine vya mitandao ya kijamii kwenye tovuti yetu.

Sheria ya Ulinzi wa- taarifa ya Uingereza inatambua kwamba aina fulani za maelezo binafsi ni nyeti zaidi. Hii inajulikana kama taarifa binafsi ‘nyeti’ au ‘kategoria maalum’ – hii inaweza kuwa kuhusu ulemavu wa mtu fulani, kwa mfano, kwa kawaida hatutakusanya maelezo haya kupitia Kitovu cha Kimataifa cha Raslimali za Uziwiupofu; hata hivyo, ikiwa uchunguzi/maswali yako yanamaanisha kwamba ni lazima tuombe maelezo hayo, tutaeleza ni kwa nini tunayaomba na jinsi tunavyokusudia kuyatumia.

Unaweza kusoma kuhusu jinsi tunavyotumia taarifa zako binafsi katika sehemu ya taarifa zako tunazifanyia nini.

Ukitupa taarifa binafsi kuhusu mtu mwingine (kwa mfano ikiwa unaomba ushauri kuhusu mwanafamilia), tutahitaji kuthibitisha kwamba umepata idhini yake ya kufanya hivyo.

Unapotumia tovuti yetu

Kama tovuti nyingi, tunatumia ‘vidakuzi’ ili kutusaidia kuboresha jinsi tunavyotengeneza, na jinsi unavyopaswa kutumia tovuti yetu. Vidakuzi vinamaanisha kuwa tovuti itakukumbuka na inaweza kutoa mtazamo wa jumla wa tabia na wingi wa wageni kwenye tovuti yetu. Unaweza kusoma kuhusu vidakuzi tunavyotumia na jinsi ya kuvidhibiti kwenye ukurasa wetu wa vidakuzi.

Ukichagua kuwasilisha maoni yako kuhusu raslimali kwa kutumia kipengele cha maoni kwenye tovuti yetu, tutahifadhi maelezo hayo kwa usalama na yatafikiwa na wafanyakazi ambao wanastahili tu. Maoni yanaweza kutolewa bila kujulikana – hakuna sharti la kujumuisha taarifa binafsi zozote na maoni yako. Maoni yote yatakaguliwa na kufutwa ndani ya mwezi mmoja tangu tarehe yalipowasilishwa.

Taarifa zako tunazifanyia nini

Tunakuhakikishia kwamba, kila wakati nia yetu ni nzuri. Ukichagua kushirikisha taarifa zako kwetu, tutazitumia ili zitusaidie kutimiza maombi yako. Ukiwasiliana nasi, tutatumia data zako kufanya mambo kama vile:

  • Tunachokifanya na taarifa unazotupa
  • Tunatoa taarifa, ambayo umeomba.
  • Tunarekodi mawasiliano yoyote tuliyo nayo ili yatusaidie kuhakikisha kwamba tunakupa mawasiliano yanayofaa zaidi,
  • Kuzuia au kugundua ulaghai au matumizi mabaya ya tovuti yetu.

Kuchambua na kutoa ripoti juu ya idadi na asili ya mawasiliano na shirika.

Tutahifadhi data zako binafsi kwa muda ambao tunahitaji kufanya hivyo, kwa kawaida ni kwa muda ambao utatuchukua kujibu ombi lolote unaloomba.

Kushirikisha taarifa zako

Tutatumia maelezo yako kwa madhumuni ambayo yanatakiwa. Kuwa na uhakika kwamba hatuuzi au kushirikisha taarifa zako binafsi kwenye mashirika mengine kwa madhumuni yao ya kujitangaza.

Hata hivyo,kuna mazingira ya nadra sana ambapo tunahitaji kushirikisha maelezo yako ikiwa ni pamoja na:

  • Ikiwa tunaamini kuwa ni muhimu kulinda au kutetea haki zetu, mali au usalama binafsi wa watu wetu au wageni kwenye majengo au tovuti zetu.
  • Pale tunapotakiwa kufanya hivyo kisheria, n.k. na wakala wa utekelezaji wa sheria inayotumia mamlaka kihalali, au ikiwa imeamliwa na amri ya Mahakama.

Pia, ikiwa utatoa maoni kuhusu matumizi yako ya Kitovu cha kimataifa cha Raslimali za uziwikutoona Duniani, tunaweza kutaka kutumia baadhi ya maelezo ambayo unatupa kutangaza tovuti yetu. Tungetarajia kutumia maoni yako bila kujulikana, lakini ikiwa sivyo, tutawasiliana nawe ili kupata idhini yako.

Msingi wetu kisheria wa kuchakata data yako

Tunahitaji msingi halali wa kukusanya na kutumia data zako binafsi chini ya sheria ya kulinda data ya Uingereza. Sheria hii inaruhusu njia sita za kuchakata data binafsi (na njia za ziada za data binafsi ambazo ni nyeti). Pili, kati ya hizi ni muhimu kwa ajili ya aina za uchakataji tunazofanya kuhusiana na Kitovu cha kimataifa cha Raslimali za Uziwiupofu duniani. Hii inajumuisha habari ambayo inachakatwa kwa misingi ya:

  • Idhini ya mtu (kwa mfano, kukutumia barua pepe au kukupigia simu).
  • Maslahi halali ya Sense (tafadhali kwa maelezo zaidi tazama hapa chini).

Data binafsi inaweza kukusanywa na kutumiwa kisheria ikiwa ni muhimu kwa maslahi halali ya shirika linalotumia taarifa hiyo, na iwapo matumizi yake ni ya haki na hayaathiri vibaya maslahi, haki na uhuru wa mtu husika.

Tunapotumia taarifa zako binafsi, kila wakati tutazingatia ikiwa ni haki na usawa kufanya hivyo na ikiwa ni kulingana na matarajio yako yanayokubalika. Tutasawazisha haki zako na maslahi yetu halali ili kuhakikisha kwamba tunatumia taarifa zako binafsi kwa njia inayofaa. Masilahi yetu halali ni pamoja na:

  • Uongozi katika Kutoa Msaada: ikijumuisha uwasilishaji wa madhumuni yetu ya hisani, ripoti za kisheria na kifedha na madhumuni mengine ya kufuata kanuni, na uhamishaji wa data baina ya vikundi.
  • Usimamizi wa Utawala na uendeshaji: ikiwa ni pamoja na kujibu maswali yaliyoombwa, kutoa taarifa na huduma, utafiti, na uchanganuzi wa taarifa.
  • Uboreshaji wa taarifa zinazohusiana na Uziwiupofu: ikiwa ni pamoja na kujibu maswali na maoni yaliyowasilishwa katika Kitovu cha kimataifa cha Raslimali za Uziwiupofu Duniani ili kutoa maudhui muhimu, yanayofaa, na yenye ubora.

Jinsi tunavyotunza taarifa zako

Tunahakikisha kwamba kuna udhibiti unaofaa wa kiufundi ili kulinda taarifa zako binafsi kwa mujibu wa sheria ya sasa ya ulinzi wa data; hii inajumuisha seva salama, ngome na usimbaji fiche wa SSL.

Kwa bahati mbaya, hakuna tovuti inayotegemea mtandao, ikiwa ni pamoja na barua pepe, iliyo salama kwa asilimia 100, ingawa tutajitahidi kadri tuwezavyo kulinda taarifazako binafsi kila wakati. Hii ni pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara wa ni nani anayeweza kufikia maelezo ambayo tumeyahifadhi ili kuhakikisha kwamba maelezo yako yanafikiwa tu na wafanyakazi wanaofaa, wafanyakazi wa kujitolea na/au wakandarasi.

Tunaweza kutumia makampuni ya nje kukusanya au kuchakata taarifa zako binafsi kwa niaba yetu. Tunafanya uchunguzi wa kina wa makampuni haya kabla ya kaunza kufanya nayo kazi na kisha tunafanya nayo kazi kwa karibu kwa muda wote wa uhusiano wetu wa kufanya kazi pamoja.

Baadhi ya wasambazaji wa tovuti hii huendesha shughuli zao katika eneo la kiuchumi la Ulaya (EEA), na hivyo wako chini ya sheria sawa za ulinzi wa data kama kampuni zilizo nchini Uingereza.

Ni kwa muda gani tunahifadhi data zako

Tunahifadhi data zako kwa muda usiotajika kulingana na umuhimu wa madhumuni ambayo data hizo zilikusanywa, kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa na Ofisi ya Kamishna wa Habari nchini Uingereza.

Urefu wa muda ambao data itahifadhiwa unategemea sababu za kuchakata data, na sheria au kanuni ambazo maelezo hayo yanaangukia.

Maoni yote kuhusu raslimali zilizowasilishwa kwa kutumia kipengele cha maoni kwenye tovuti yatakaguliwa na kufutwa ndani ya mwezi mmoja tangu tarehe ambayo yaliwasilishwa.

Ukiomba kutopokea mawasiliano zaidi kutoka kwetu, ingawa tutalishughulikia hilo, tutaweka baadhi ya taarifa za msingi kukuhusu kwenye orodha ili kutuwezesha kutii ombi lako.

Haki zako

Una haki nyingi chini ya sheria ya ulinzi wa data ya Uingereza. Ikiwa ungependa kutumia mojawapo ya haki hizi au kuzijadili zaidi, tafadhali wasiliana na Timu ya Huduma za Wasaidizi ambao maelezo yao yametolewa kwenye ilani hii na katika sehemu ya Jinsi ya kuwasiliana nasi.

Haki zako kuu ni:

  • Uwazi juu ya jinsi tunavyotumia taarifa zako binafsi (haki ya kufahamishwa). Ilani hii ya faragha, pamoja na maelezo yoyote ya ziada ambayo umepewa wakati ulipotoa maelezo yako, au baadaye, inakusudiwa kukupa maelezo haya.
  • Omba nakala ya maelezo tuliyo nayo kukuhusu – hili wakati mwingine huitwa ombi la ufikiaji wa somo la taarifa (haki ya ufikiaji). Tutatoa haraka iwezekanavyo, taarifa yoyote inayokuhusu ambayo tumehifadhi ambayo utaiomba, lakini hili linaweza kuchukua hadi siku 30. Hatutakutoza kwa hili isipokuwa katika hali za kipekee. Kwa kawaida utaombwa uthibitisho wa utambulisho kwani tunahitaji kuwa na uhakika kwamba tunakutolea tu data yako binafsi.
  • sahihisha au urekebishe maelezo tuliyo nayo kukuhusu ikiwa si sahihi (haki ya urekebishaji).
  • Utuombe tuache kutumia maelezo yako (haki ya kuzuia uchakataji). Katika hali fulani, una haki ya kuomba uchakataji wa data yako binafsi uzuiliwe kwa sababu kuna kutokubaliana kuhusu usahihi au matumizi yake halali.
  • Utuombe tuondoe taarifa zako binafsi kutoka kwenye rekodi zetu (haki ya ‘kusahauliwa’) Kumbuka: pale ambapo umeomba tusikutumie raslimali za matangazo, tutahitaji kuweka baadhi ya taarifa chache ili kuhakikisha kwamba hutawasiliana na yajayo.
  • Ondoa idhini yako. Ambapo tunachakata data yako kulingana na idhini yako (kwa mfano, kukutumia maandishi ya matangazo au barua pepe), unaweza kuondoa idhini hiyo wakati wowote.
  • Pingamizi la uchakataji wa taarifa zako kwa madhumuni ya matangazo (haki ya kupinga). Pia una haki ya kutuzuia kuchakata data ambazo tunategemea zipo ndani ya maslahi yetu halali kufanya hivyo (kwa mfano, kukutumia matangazo ya moja kwa moja kwa njia ya posta).
  • Pata na utumie tena data yako binafsi kwa madhumuni yako mwenyewe (haki ya uchukuliaji wa data).
  • Kutokuwa chini ya uamuzi ikiwa ni msingi wa uchakataji wa kiotomatiki (ufanyaji maamuzi na uwekaji wasifu kwa kujiendesha kiotomatiki).

Ikiwa una uhakika kuwa tumechakata data yako kwa mujibu wa notisi hii au ungependa kulalamika, tafadhali wasiliana na Timu yetu ya Huduma za Wasaidizi kwa mara ya kwanza.

Iwapo hujaridhika na jibu letu au unaamini kuwa hatuchakati data yako binafsi kwa mujibu wa sheria, unaweza kuwasiliana na Ofisi ya Kamishna wa Habari (ICO) nchini Uingereza:

Ofisi ya Kamishna wa Habari (Uingereza)

Nambari ya usaidizi: 0303 123 113

Tovuti: https://ico.org.uk/global/contact-us/

Jinsi ya kuwasiliana nasi

Ikiwa wakati wowote ungependa tubadilishe namna ya kuwasiliana nawe, tafadhali wasiliana na Timu yetu ya Huduma za Wasaidizi.

Barua pepe: [email protected]

Chapisho: Timu ya Huduma za Wasaidizi, Sense, 101 Pentonville Road, London, N1 9LG, Uingereza

Taarifa za faragha

Notisi hii ya Faragha ilisasishwa mara ya mwisho Machi 2024 [email protected]

Huenda Sense International ikahitaji kufanya mabadiliko kwenye notisi hii ya faragha mara kwa mara. Ikiwa tutafanya mabadiliko yoyote muhimu na kwa jinsi tunavyoshughulikia maelezo yako binafsi tutaliweka hili wazi kwenye tovuti ya Kitovu cha kimataifa cha Raslimali za Uziwiupofu Duniani au pengine kwa kuwasiliana nawe moja kwa moja. Tafadhali tembelea tovuti ya Kitovu cha Kimataifa cha Raslimali za Uziwipofu Duniani mara kwa mara ili kupata toleo jipya zaidi na utufahamishe ikiwa utakuwa na maswali au wasiwasi wowote.

Tafadhali kumbuka kwamba notisi hii ya faragha inatumika kwenye tovuti ya Kitovu cha kimataifa cha Raslimali za Uziwiupofu Duniani. Notisi za faragha zinazotumika kwenye tovuti za Sense na Sense International zinatofautiana na notisi hii ya faragha. Ukifikia tovuti za Sense au Sense International kwa kujitegemea au kupitia viungo vya Kitovu cha kimataifa cha Raslimali za Uziwiupofu Duniani, utahitaji kukagua taarifa za faragha kwenye tovuti hizi ili kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi taarifa zako binafsi zinavyokusanywa, kuhifadhiwa na kutumiwa.