Je, hii inamfaa nani?

Waalimu, Wanafunzi, Wazazi, Watunga sera na Wasimamizi

Mwaka wa kuchapishwa
June 2025
Imetengenezwa na
Sense International Tanzania

Angel na Kelvin ni watoto wanaoishi na ulemavu wa uziwikutoona, video inaelezea namna wanavyowahudumia watoto wao na namna walimu wanavyowasaidia kuwafundisha.

Maelekezo elekezi ya video

Maelezo Picha:

Taaribu Kelvin anacheza mwenyewe kwenye mazingira ya bustani ya nyumbani kwa kurusha mikono yake huku na kule huku maandishi yanatokea yakisomeka ‘My name is Kelvin, It’s a beautiful day but I can’t see or hear’.

Mama Kelvini: Kelvi alikuwa hajui kula mwenyewe, alikuwa anajisaidia mwenyewe kwenye nguo.

Maelezo picha:

Mama yake Kelvin amekaa anaongea mbele ya mti unaoonekana kwa mbali.

Teddy Andrew: kwa kweli alivyozaliwa hali yake nilikuwa namuona tu mama yake ana mbeba, mimi hadi mtoto wangu akaanza kutembea yeye bado tu anambeba hadi nikamuuliza mbona huyo mtoto una mbeba sana? Kwa nini asitembee? Akaniambia kwamba mimi mwanangu haoni. Nilishituka sana.

Maelezo picha:

Mwanamama amekaa nje kwenye eneo la wazi anaongea. Kelvin amekaa kwenye kiti eneo la nje. Kelvin anashikwa mkono na mwalimu wake wakiwa darasani. Mtoto mtoto ameengea kiti huku akionekana anawaza jambo kwa kina.

Angel amekaa mlangoni akiwa amegeuka nyuma, maneno yanatokea kwenye skrini yakisema ‘My name is Angel, I can’t hear and I cant talk. Kamera inamuonyesha Angel kwa karibu akiwa anashangaa jambo.

Baba yake Anjelina: Kwanza Anjelina alikuwa hakai, tukaanza kutafuta vifuko vya mchana kumuweka kwenye kiuno kusudi akae.

Maelezo picha:

Baba yake Angel amekaa karibu na ukuta wa nyumba akiongea.

Fatma Yusufu: Historia yake ni kuwa alifichwa ndani kabisa Angel alifungiwa ndani alikuwa haonekani.

Maelezo picha:

Fatma Yusuph amekaa kwenye mazingira ya shule akiongea, nyuma yake kwa mbali kuna miti ya bustani.

Mama Angel: Mimi nilikuwa sitoki nae nje kwa sababu naongopa watu watanicheka, na hata mtu akiniona ananiambia nimemroga mtoto wangu lakini sio hivyo.

Maelezo picha:

Mama Angel amekaa mbele ya ukuta wa nyumba akiongea.

Kelvini anainama huku kamera ikionyesha miguu yake.

Kelvin amekaa pembeni mwa meza kwa utulivu.

Bibi yake Kelvini: Mama kaanza kumwaga zege mtoto akiwa na miezi miwili, mtoto nikawa nipo nae mimi. Hadi amekuja kufikia miaka mitano mama sasa ndio akapata ushauri wa watu kuwa huyu mtoto sio mlemavu sio masikini uwezo upo wa kumpeleka shule.

Maelezo picha:

Bibi yake Kelvin ameshika mtoto mdogo wamekaa kwenye kiti.

Bibi yake Kelvini amekaa kwenye kiti karibu na mti akiongea. Maandishi yenye jina lake yanatokea kwenye skrini yakisomeka ‘Maria Zacharia’.

Kelvini amesimama na mama yake akicheza.

Yanatokea maandishi yanasema ‘Shirika la Sense International Tanzania limesaidia watoto 100 wenye uziwikutoona na ulemavu mchanganyiko kusoma nchini Tanzania kwa kuwasomesha wasaidizi wa walimu 100 kufanya kazi na walimuu wa shule kwenye madarasa jumuishi’

Watoto wanaimba,na Kelvin nae, tunampenda sana, na Angel nae tunampenda sana.

Mwalimu anamsaidia Kelvin kupanda kwenye ngazi za kuingia darasani.

Watoto wemekusanyika wakicheza pamoja na Kelvin kwenye mduara huku Kelvin ameshikwa mikono na mwalimu wake.

Angel amekaa kwenye kiti huku ameshikiliwa na mwalimu wake, watoto wamemzunguka wakiendela kuimba na kurukaruka wakipiga makofi.

Angel ameshikwa mkono na mwalimu wake huku watoto wenzake wakimuangalia kwa furaha.

Fatma Yusufu: Ratiba zetu za shule kwa sisi darasa la awali tunaanza na mduara katika kuimba na kufurahi na watoto wengine tunacheza na yeye anakuwa kama watoto wenzake.

Maelezo picha:

Mwalimu wake Angel amekaa kwenye kiti akiongea, pembini yanatokea maandishi yakisomeka Fatma Yusufu, mwalimu msaidizi.

Yusebi John: Wenzeka wanaposoma ratiba imebandiwa mahala kwa sababa wao wanaona yeye kwa sababu ana upungufu wa kutoona yeye ratiba yake anaisoma kwa kugusa.

Maelezo picha:

Yusebi John amesimama anaongea, pembeni yanatokea maneno yanasomeka jina lake Yusebi John, mwalimu msaidizi.

Kelvin amesimama mbele ya darasa huku ameshikwa mikono na mwalimu wake, wanafunzi wenzake wamekaa chini wakimuangalia kwa furaha.

Fatma Yusufu: Wakati mwalimu anaenda ubaoni kuwafundisha watoto wengine kuhesabu sisi huwa tuna vifuniko au vizibo au vihesabio vya aina yoyote na kikombe au kibakuli, Angel anaweza mwenyewe kuokota vidude na kwa kumuongoza.

Maelezo picha:

Mwalimu wake Angel amekaa kwenye kiti akiongea, pembini yanatokea maandishi yakisomeka Fatma Yusufu, mwalimu msaidizi.

Mwalimu anapiga makofi mbele ya darasa huku wanafunzi wakimuangalia.

Mwalimu anamshika mkono Angel kumfundisha namna ya kuhesabu kwa kutumia vizibo vya chupa.

Mwalimu ameshika Angel mkono huku akimuelekeza namna ya kuhesabu.

Edina Leonard: Nashukuru kwa kuwa na mwalimu msaidizi, kwa kweli bila mwalimu msaidizi nisingeweza peke yangu. Mwalimu msaidizi amekuwa msaada sana kwa sababu nisingeweza kumuhudumia Angel kwa uhitaji ule alionao nikaweza kuwahudumia na hawa watoto wengine.

Maelezo picha:

Edina Leonard amekaa kwenye dawati darasani, kwenye skirini pembeni maneno yenye jina lake yanatokea yakisomeka Edina Leonard, mwalimu.

Mwalimu akiwa darasani pamoja na wanafunzi, anamsaidia Angel kuandika huku mwanafunzi mwingine akiwa pembeni yake akimsaidia pia.

Edina Leonard amekaa kwenye dawati darasani.

Mwalimu yupo darasani anawafundisha watoto kusoma, nyuma yake kuna ubao wa darasani umeandikwa a,e,I,o,u.

Mama yake Angel: Walimu wasaidizi wamesaidia sana kwa sababu wakati nampeleka Angel shule alikuwa hawezi kukaa, kuna maneno alikuwa hawezi kutamka, lakini nashukuru nilivyompeleka shule mtoto wangu alibarika ghafla.

Maelezo picha:

Mama Angel amekaa mbele ya ukuta wa nyumba akiongea.

Angel amekaa chini kwenye sakafu anacheka kwa furaha.

Fatma Yusufu: Mimi mwenyewe nilikuwa mbishi katika hili swala kusema kwamba huyu Angel anaweza kubadilika. Nilivyompokea kama mtoto mchanga lakini mpaka hii leo kila mtu anashangaa Angel anaweza kuandika, Angel anaweza kufanya hivi. Hata mama yake mwenyewe anasema hawa Sense Mungu tu awalinde.

Maelezo picha:

Mwalimu yupo pamoja na wanafunzi darasana wakicheza na kushangalia kwa kuimba.

Mwalimu wake Angel amekaa kwenye kiti akiongea, pembini yanatokea maandishi yakisomeka Fatma Yusufu, mwalimu msaidizi.

Angel amekaa kwenye dawati lake darasani, rafiki yake anakuja anamuelekeza jambo.

Mama yake Kelvini: Kelvini tangu ameenda shule kuna mabadiliko na kule pia anakula nashika kikombe anakula mwenyewe yani imenisaidia, hata walimu nawashukuru wapo vizuri kwa mtoto wangu.

Maelezo picha:

Mama yake Kelvini amekaa kwenye kiti chini ya mti, pembeni yake kwenye skrini yanatokea maneno yanasomeka Ruth Cornel,  Kelvin’s mother.

Kelvini amekaa amenyoohsa miguu akinywa juisi.

Watoto wanatoka darasani kwa kukimbia kwa furaha, Kelvin anatoka akitembe kwa kusaidiwa na wanafunzi wenzake.

Mama yake Kelvini: Ninapotoka nae shuleni narudi nyumbani, nampa chakula ana pumzika, akishaamka naanza kumfundisha hiyo tablet kwa sababu yeye ulemavu wake ni wa kutokuona na kusikia, anasikia tu kwa mbali. Kwa hiyo pale katika kumfundisha kwenye hiyo Tablet namuwekea nyimbo za kufundisha za mtoto.

Katika ile simu ukimfungulia ukimfungulia vitu akisikia maneno na yeye anakalili, anaweza kukwambia toka, anaweza kukwambia njoo, anawezakukwambia bye. Na pia imenisaidia mambo mengineyo anapokuwa shuleni mimi mwenyewe nafanya shughuli zangu kama na safari zangu natoka.

Maelezo picha:

Mama yake Kelvini anacheza na Kelvini huku mwalimu wake Kelvini akiwaangalia huku anafurahi.

Kelvni amebebwa na mama yake ambaye amekaa kwenye kiti akiongea.

Kelvin anaka kwenye kiti na mama yake ambaye ameshika kishikwambi, anamuweka miguu vizuri na kumuwekea kishikwambi kwenye sikio. Kelvini anafurahi na kurusha mikono.

Angel amekaa kwenye dawati lake akiwa na kishikwambi

Fatma Yusufu: Yani huu mradi wameuanzisha waliona mbali sana kuanzisha mradi kama huu kwa sababu kuna watoto wengi ambao walifichwa ndani kama Angel. Historia yake ni kuwa alifichwa ndani kabisa, Angel alifungiwa ndani alikuwa haonekani na kuna walemavu wengine baada ya kuwaona hawa kina Angel wanakuja shuleni basi na wao walitamani walikuja wengi na wengine tukawapeleka huko Sense.

Maelezo picha:

Walimu wamekaa na Angel kwa pamoja wakipiga picha ya kumbukumbu.

Angel amesimamishwa kwenye kiti pembeni wanafunzi wenzie wamesimama wakifurahi.

Mwalimu wake Angel anaongea kisha maneno yenye jina lake Fatma Yusuph, mwalimu msaidizi yanatokea.

Mama yake Kelvini: Yaani mradi umenisaidia sana sijui nielezeeje, chakuwapa mimi sina ni shukrani na nilikuwa naomba wasiishie hapa, iwe endelevu kwa mtoto wangu.

Maelezo picha:

Mama yake Kelvi amekaa chini anaongea.

Kelvini amebebwa na mwalimu wake huku anarushwarushwa juu kwa kucheza na Kelvini anafurahi.

Kelvini amesimama na rafiki zake wawili huku amemkumbatia mmoja na mwingine pembeni amesimama.

Angel anachungulia mlangoni.

Skrini inakuwa nyeupe kisha nyeusi kisha chapa za Human Development Innovation Fund, Sense International na UKAid zinatokea.

Je, hii ilifaa

Maelezo haya yamekusaidia?Inahitajika
This field is for validation purposes and should be left unchanged.

Changia


Raslimali zinazofanana

Festo – Kijana mwenye uziwikutoona, Tanzania

Video ya kijana mwenye uziwikutoona akijiingizia kipato kwa kufanya shughuli ya utengenezaji wa vikapu.

Philbert – Kijana mwenye uziwikutoona kutoka Tanzania

Ujumuishaji wa vijana wenye uziwikutoona kwenye shughuli za kiuchumi.

Kuweka mwenekano wa darasa kwa ajili ya wanafunzi wenye Uziwikutoona 

Namna ya kuliandaa darasa kuwa mazingira rafiki kwa wanafunzi wenye uziwikutoona.