Sense International ni shirika la hisani linaloongoza ulimwenguni katika kuwasaidia watu wenye uziwikutoona katika nchi nane duniani.
Kazi yetu inalenga katika kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wa uziwikutoonawanaweza kupata elimu, huduma za afya na kazi, ili waweze kustawi na kuishi maisha kwa uwezo wao kamili.
Kwa kufanya kazi moja kwa moja na watu walio na uziwikutoona, tunataka kwenda nje ya mipaka ya nchi zetu nane, tukiwasaidia kutangamana na wengine na ulimwengu unaowazunguka.
Kitovu cha kimataifa cha raslimali za uziwikutoona Ulimwenguni kinapatikana katika lugha saba tofauti na kina rasilimali nyingi zinazoshughulikia mada anuwai ikiwa ni pamoja na elimu, haki za ulemavu na ustawi.