Nchini Nepal, inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 11,500 wanaishi na uziwikutoona.
*Shirikisho la uziwikutoona Duniani, 2018 Katika hatari ya kutengwa kwenye utekelezaji wa CRPD na SDGs: Kutokuwepo kwa usawa kwa watu wenye uziwikutoona.
Nchini Nepal, watu walio na Uziwikutokuona wanachukuliwa kuwa miongoni mwa vikundi vilivyotengwa na vilivyo hatarini zaidi.
Kulingana na ufafanuzi wa awali wa Serikali ya Nepal na uainishaji wa ulemavu, uziwikutoona ulizingatiwa kuwa ni aina nyingine tu katika kategoria ya ulemavu wa aina nyingi. Hii ilifanya iwe vigumu kwa watu wenye uziwikutoona kupata msaada mahususi na usaidizi waliohitaji.
Shukrani kwa utetezi uliofanywa na jumuiya inayoongozwa na Shirikisho la Kitaifa la Walemavu la Nepal [NFDN], serikali ilitenganisha ulemavu wa uziwikutoona kutoka katika kundi la ulemavu wa aina nyingi na kutambua kuwa ni ulemavu tofauti mwaka 2006. Hata hivyo, pamoja na utambuzi huu, watu wenye ulemavu wa uziwikutoona bado wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kupata taarifa, kupata haki zao, na kupata usaidizi wanaohitaji.
Ufikiaji wa teknolojia unaweza kuwa chanzo cha mabadiliko kwa watu wenye ,uziwikutoona kutoa njia mpya za kupata habari, kuwasiliana na watu wengine, na kushiriki kikamilifu katika maisha ya kila siku.
Raslimali hizi zitawawezesha watu wenye uziwikutoona na wale wanaowasaidia kuishi, kujifunza, na kustawi.