Nchini Peru, inakadiriwa kuwa watu 650,000 wanaishi na aina yauziwikutoonamdogo na takriban watu 65,000 wanaishi na aina uziwikutoona mkali.*
*Shirikisho la uziwikutoona Duniani, 2018 Katika hatari ya kutengwa kwenye utekelezaji wa CRPD na SDGs: Kutokuwepo kwa usawa kwa watu wenye uziwikutoona.
Ulemavu wa uziwikutoona unatambuliwa kama ulemavu wa kipekee na huweka masharti kwa ajili ya kuwatunza watu wenye . uziwikutoona Sheria ya Peru Na. 29524 (2010) inafafanua :uziwikutoona
Ulemavu unaodhihirishwa na ulemavu wa kusikia na kuona kwa wakati mmoja, kwa kiwango cha sehemu au yote kwa pamoja, kwa njia tosherevu na makini katika mwafaka wa mawasiliano, uhamasishaji na ufikiaji wa habari na mazingira.
Fasili hii inamaanisha kwamba sio tu unachukuliwa kuwa ni ulemavu wa pande mbili, pia inazingatia mahitaji yao ya jumla kama mtu. Ingawa fasili hii inaashiria mafanikio, lakini bado maendeleo yamekuwa ni ya polepole kuhusu upatikanaji wa huduma, upatikanaji wa mawasiliano na au mafunzo na utangamano katika soko la ajira.
Sensa ya kitaifa ya mwaka 2017 iligundua kuwa idadi ya watu wanaoishi na ulemavu nchini Peru wana viwango vya chini vya elimu. Asilimia 14% ya watu wenye ulemavu hawajafikia kiwango chochote cha elimu, na asilimia 32% hawajasoma zaidi ya shule ya msingi. Kwa wale ambao wamepata fursa ya kupata elimu, mara nyingi shule hazijaandaliwa vya kutosha kuweza kuwajumuisha, huku walimu wengi wakihisi hawajapewa mafunzo ya kuwawezesha kutoa elimu bora.
Watu wenye uziwikutoona bado wametengwa na wanahitaji kupata msaada ambao ni mahususi kwa ajili ya mahitaji yao ili waweze kuonekana na kushiriki kikamilifu zaidi katika jamii zao.
Ufikiaji wa teknolojia unaweza kuwa chanzo cha mabadiliko kwa watu wenye ,uziwikutoona kutoa njia mpya za kupata habari, kuwasiliana na watu wengine, na kushiriki kikamilifu katika maisha ya kila siku.
Raslimali hizi zitawawezesha watu wenye uziwikutoona na wale wanaowasaidia kuishi, kujifunza, na kustawi.