*Shirikisho la  uziwikutoona Duniani, 2018 Katika hatari ya kutengwa kwenye utekelezaji wa CRPD na SDGs: Kutokuwepo kwa usawa kwa watu wenye  uziwikutoona. 

 Watu wenye  uziwikutoona nchini Uganda mara kwa mara wanakumbana na vikwazo vingi huku pia wakikabiliana na changamoto za mapungufu ya mawasiliano. Katiba ya Jamhuri ya Uganda ya mwaka 1995 inahakikisha haki ya usawa na uhuru kutoka kwenye ubaguzi.

Sera ya TEHAMA kwa watu wenye ulemavu nchini Uganda inaelezea TEHAMA kama mawasiliano ambayo yanajumuisha lugha, maonyesho ya maandishi, Braila, mawasiliano ya kugusa, maandishi makubwa, medianuwai zinazoweza kufikiwa na vile vile maandishi, sauti, lugha nyepesi. Lengo kuu la Sera ya TEHAMA kwa watu wenye ulemavu ni kutumia TEHAMA kama hatua ya kupunguza kuwatenga watu wenye ulemavu na kuunda fursa sawa kwa kuziba mapengo ya upatikanaji na matumizi ya zana za TEHAMA.

Tume ya Mawasiliano ya Uganda imepewa mamlaka chini ya kifungu cha 5 cha (Sheria ya Mawasiliano ya Uganda 2013) kuendeleza utafiti katika uundaji na utumiaji wa teknolojia mpya ikijumuisha zile ambazo zinahimiza ufikiaji wa huduma ya mawasiliano kwa watu wenye ulemavu. Kwa muda mrefu, hali hii imekuwa moja ya vikwazo vikubwa kwa watu wenye Uziwikutokuona katika kupata huduma.

Ufikiaji wa teknolojia unaweza kuwa chanzo cha mabadiliko kwa watu wenye ,uziwikutoona kutoa njia mpya za kupata habari, kuwasiliana na watu wengine, na kushiriki kikamilifu katika maisha ya kila siku.

Raslimali hizi zitawawezesha watu wenye uziwikutoona na wale wanaowasaidia kuishi, kujifunza, na kustawi.