*Shirikisho la  uziwikutoona Duniani, 2018 Katika hatari ya kutengwa kwenye utekelezaji wa CRPD na SDGs: Kutokuwepo kwa usawa kwa watu wenye  uziwikutoona. 

 Uziwikutoona unafafanuliwa katika muktadha wa Kihindi katika ‘Sheria ya Haki za Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2016’ kama “hali ambayo mtu anaweza kuwa na mchanganyiko wa ulemavu wa kusikia na kuona na kusababisha matatizo makubwa ya mawasiliano, maendeleo na elimu”. Kuna zaidi ya watu 500,000 wanaoishi na uziwikutoona nchini India, na kuna idadi ndogo tu ya mashirika ambayo yamejitolea kusaidia idadi hii.

Huko nyuma, mnamo mwaka1997, kulikuwa na shule moja tu nchini India ambayo ilikuwa ikitoa elimu na huduma zingine kwa watoto 23 wenye Uziwikutokuona.

Hivi sasa Sense India inafanya kazi katika majimbo 23 ya India kupitia mtandao wa NGOs wa shirika zipatazo 60, kubadilisha maisha ya zaidi ya watu 80,000 wenye uziwikutoonakutoka kutengwa na kupuuzwa hadi kuuelewa ulimwengu wao na kuishi maisha kamili na hai.

Ufikiaji wa teknolojia unaweza kuwa chanzo cha mabadiliko kwa watu wenye ,uziwikutoona kutoa njia mpya za kupata habari, kuwasiliana na watu wengine, na kushiriki kikamilifu katika maisha ya kila siku.

Raslimali hizi zitawawezesha watu wenye uziwikutoona na wale wanaowasaidia kuishi, kujifunza, na kustawi.