Je, hii inamfaa nani?

• Waalimu
• Wanafunzi
• Wazazi
• Watunga sera
• Wasimamizi

Mwaka wa kuchapishwa
February 2026
Imetengenezwa na
Sense International Tanzania

Mama Mahdi ni mmoja wa wazazi wanaotumia Global Deafblindness Resource Hub. Anaeleza athari za Kituo hicho na jinsi ambavyo kimebadilisha maisha yake.

Manukuu wa video ya Mama Mahdi

Mama Mahadi

Kwa majina naitwa mama Mahdi nina mtoto mwenye changamoto ya mgongo wazi na pia na kichwa kikubwa, mimi ni mtumiaji wa hii Global Resource (Deafblindness) Hub na imenipa manufaa makubwa.

Video inayoonekana

Kutoka juu kamera inaonesha eneo kubwa la mtaa anaoishi mama Mahadi, kamera inasogea kumfuata alipo, mama Mahadi anatembea kuelekea nyumbani kwake amemshika Mahad.

Mama Mahid

Sehemu zenye manufaa makubwa kwangu kwenye Global Resource (Deafblindness) Hub ni zile sehemu zilizochanganua elimu ya uziwikutoona, kuna hatua za kumtambua mtoto mwenye uziwikutoona endapo utakuwa nae nyumbani.

Video inayoonekana

Mama Mahad amekaa chini na mtoto wake kamshika mkononi huku akiwa anatumia simu yake kuperezi kitovu cha kimataifa cha rasilimali za uziwikutoona. Kamera inasogea kumfuata kwa karibu. Mama Mahad amekaa kwenye sofa sebuleni anaaongea kuhusu kitovu cha kimataifa cha rasilimali za uziwikutoona. Kamera inaonesha kwa karibu simu ya mama Mahad.

Mama Mahad

Global Resource (Deafblindness) Hub imenisadia kwa kiwango kikubwa sana, kwa sasa nimepata elimu ya kumtambua mtoto mwenye changamoto hiyo [uziwikutoona] endapo nitakuwa nae, nina elimu ya kumjua haraka na kumsaidia ili awe sawa kama watoto wengine.

Video inayoonekana

Kamera inasogea kumfuata kwa karibu Mama Mahadi akiwa ameshika simu anaangalia kitovu cha kimataifa cha uziwikutoona.

Mama Mahad

Global Resource (Deafblindness) Hub haitoi tu elimu peke yake bali imekuwa ikitoa msaada mkubwa kwa jamii, kati ya wazazi na watoto ili kuipata ile elimu [ya uziwikutoona] kwa haraka, wazazi wengi wamekuwa na elimu ya kutosha kupitia huu mtandao wa Global Resource (Deafblindness) Hub kwa hiyo imesaidia sana kwa kiwango kikubwa. Na pia imekuwa daraja kubwa la kuunganisha kati ya mama mwenye mtoto na kupata ile elimu kwa uharaka zaidi.

Video inayoonekana

Mama Mahad amemshika mtoto wake huku upande mwingine ameishika simu yake, kamera inasogea kurudi nyuma kutoka alipo Mama Mahad. Mama Mahad amekaa kwenye kiti sebuleni anaongea kuhusu kitovu cha kimataifa cha uziwikutoona.

Mama Mahad

Rasilimali ambazo ningependa ziongezwe, zipo rasilimali tofauti tofauti ambazo nimezielewa na zingine ningependa ziongezwe na ziboreshe ili Global Resource (Deafblindness) Hub iwe kwa upana zaidi, elimu ya afya ya mama ya uzazi na mtoto hii ingewekwa na mchango mkubwa sana wa kumfanya mama ajue ni vitu gani anatakiwa kufanya wakati akiwa na ujauzito ili ampate mtoto mwenye afya iliyo bora.

Video inayoonekana

Kamera inamfuata mama Mahad akiwa ameshika simu yake na mtoto wake wakitumia kitovu cha kimataifa cha rasilimali za uziwikutoona.

Mama Mahad

Ingependeza zaidi changamoto zingine ambazo hazihusiani na uziwikutoona zingewekwa pia kwenye Global Resource (Deafblindness) Hub kwa mfano kuna ulemavu wa mgongo wazi, kuna kichwa kikubwa na kadhalika, hivi vitu vingewekwa ingekuwa na mchango mkubwa sana kwa wazazi na kujua ni namna gani ya kufanya.

Video inaoyoonekana

Mama Mahad amekaa kwenye kiti anaongea, akitumia lugha ya mwili hapa na pale. Kamera inamfuata mama Mahad akiwa ameshika simu yake na mtoto wake wakitumia kitovu cha kimataifa cha rasilimali za uziwikutoona.

Mama Mahad

Naweza kusema Global Resource (Deafblindness) Hub imenibadilisha vitu vingi, kwanza, nimeondoa hofu na mashaka ya kulichukulia tatizo la ulemavu kama mzigo lakini baada ya kupata elimu nimeona hili tatizo ni la kawaida na mtoto anaweza kuishi kama mtu mwingine tu wa kawaida kwa hiyo imenijengea moyo na imani na ujasiri kwamba hili tatizo lipo na linaweza likatatulika kwa namna nyingine.

Video inayoonekana

Mama Mahad amekaa kwenye kiti. Inaingia inaonekana video ya mama Mahad akiwa anatumia simu yake. Mama Mahadi amekaa na mtoto wake huku anatumia simu yake ya mkononi. Mama Mahadi anaonekana amekaa kwenye sofa lake sebuleni anahojiwa kuhusu kitovu cha kimataifa cha uziwikutoona.

Je, hii ilifaa

Maelezo haya yamekusaidia?

Changia


Raslimali zinazofanana

Mchezo Wa Mjongeo Na Hisia Kwa Watoto Wenye Uziwikutoona: Seti Ya Zana Kwa Mtoa Huduma

Rasilimali hii inatoa mwongozo hatua kwa hatua kuhusu kutumia michezo na shughuli za mwendo—kama vile kuzungusha, bakuli za hisia, na michezo ya mpira—kusaidia maendeleo ya mwili, hisia, na kijamii kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuona.

Marekebisho ya Darasa kwa Ajili ya Wanafunzi Wenye Uziwikutoona

Rasilimali hii inatoa mwongozo juu ya jinsi ya kufanya marekebisho ya darasani kwa watoto wenye ukosefu wa macho na kusikia.

Muziki Na Mjongeo Kwa Watoto Wenye Uziwikutoona: Mwongozo Wa Vitendo

Mwongozo huu unatoa njia za vitendo kwa walei na walimu kutumia muziki na mwendo kusaidia kujifunza, mawasiliano, na ujumuishaji kwa watoto wenye ukosefu wa kuona na kusikia.