Je, hii inamfaa nani?

• Wanafunzi
• Wazazi
• Watunga sera

Mwaka wa kuchapishwa
May 2026
Imetengenezwa na
Sense International Tanzania

Inaelezea ni kwa namna gani darasa la wanafunzi wenye uziwikutoona linabidi lipangiliwe na kila kifaa cha kujifunzia namna kinatakiwa kuwekwa mahali pake.

Manuscripti ya video

Madam Maula ameketi darasani, baadhi ya vifaa vya kufundishia kama ubao vinaonekana kutoka nyuma. Anazungumza kwa kujiamini huku akiangalia kwenye kamera akieleza jinsi darasa la wanafunzi uziwikutoona linavyopaswa kuonekana.

Madam Maula
Darasa la viziwi wasiion, unaweza kwa sababu mwalimu ni mmoja na mwanafunzi ni mmoja. Kwa hiyo unaweza ukaweka kona darasa, mwalimu utakaa na mtoto utamfundisha, kama ni mtoto mwenye uziwikutoona bila baki ya usikivu au uoni, yule atategemea sana mikono yako kwa hiyo inabidi ukae nae karibu, kwa hiyo ile chema itamsaidia kwa kuwa utakuwa nae karibu pamoja.

Kama mwalimu unatka kuweka vifaa kwenye darasa, darasa la viziwi wasioona vifaa vyake havitakiwi kuhamishwa, kwa mfano, tunaanza kumfundisha mtoto abaini darasa lake, tuna reli za kuingilia darasani, baada ya reli, mlangoni lazima uweke kitu ambacho atafahamu mlango wa kuingia ni upi, atagusa, akishagusa kitu kinachofuatia ni nini? Labda kitu kinachofuati kutoka pale atakapotoka nitaweka labda meza, kwa hiyo atagusa meza, akigusa meza, akitoka meza anajua naingia katika dawati lang au kiti changu ninachokaa kwa hiyo hataweza kupotea.

Sasa kama mwalimu atahamisha ile meza atashindwa kubaini darasa kwa sababu ataingia akigusa meza haini ukumbuke kuwa huyu haoni kwa hiyo lazima wanapobaini darasa lake lazima uweke vitu ambavyo vitamkumbusha kwamba mimi natakiwa nikae pale.

Labda anataka kutumia mashine, mashine ile utaiweka sehemu ambayo yeye ataweza kutambua ni sehemu gani naweza nikapta mashine ya kuchapia. Kuna matumizi ya kompyuta, pia lazima uiweke sehemu ambayo yeye atabaini kompyuta hii iko wapi kwa kufuata hivyo vigezo. Aidha tunaweza kumuwekea bata kamba darasani, akigusa kamba anaweza kufika kwenye kompyuta ikawea ni rahisi yeye kwenda bila kumuelekeza. Nikikata kushoto, naweza nikaona kompyuta, hapa nilipokaa nikikata kushoto kuna kompyuta. Kwa hiyo mtoto utakuwa umeshamgusisha, na haya mazoezi sio ya siku moja unaweza kuchukua siku nyingi yanakuwa mazoezi ya kudumu ili mtoto ajue sehemu yake ya kukaa. Anajua nikiingia darasani nagusa kitu fulani naingia darasani. Na nikishaingia mlangoni niguse nini ili nifike katika dawati langu, au nitagusa nini ili nifike kwenye kompyuta yangu au nifike kwenye mashine yangu ya braili mtoto atajua au kitabu. Nitafika sehemu gani nitafute kitabu na ukifundisha utamuacha mwenye akirudishe palepale.

Kwa hiyo hata shelfu zetu zinakuwa na sehemu ambazo mtoto atajua sehemu ya kwanza, kitabu hiki hakikai hapa, sehemu ya pili hiki kitabu ndio nakipata. Akimaliza kusoma anaenda kushika sehemu ya kwanza, hapana, sehemu ya pili ndio nakipanga. Kwa hiyo vitu vyao vinakuwa katika utaratibu uliowekwa. Tofauti na madarasa mengine ukiamisha utaratibu huo lazima umuamishe mtoto, umueleze.

Je, hii ilifaa

Maelezo haya yamekusaidia?

Changia


Raslimali zinazofanana

Namna ya kumfundisha mwanafunzi mwenye uziwikutoona

Video ya mwalimu wa kitengo maalumu akielezea namna kumfundisha mwanafunzi mwenye uziwikutoona.

Mchezo Wa Mjongeo Na Hisia Kwa Watoto Wenye Uziwikutoona: Seti Ya Zana Kwa Mtoa Huduma

Rasilimali hii inatoa mwongozo hatua kwa hatua kuhusu kutumia michezo na shughuli za mwendo—kama vile kuzungusha, bakuli za hisia, na michezo ya mpira—kusaidia maendeleo ya mwili, hisia, na kijamii kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuona.

Marekebisho ya Darasa kwa Ajili ya Wanafunzi Wenye Uziwikutoona

Rasilimali hii inatoa mwongozo juu ya jinsi ya kufanya marekebisho ya darasani kwa watoto wenye ukosefu wa macho na kusikia.