Jinsi ya kukifanya kifaa chako kiweze Kufikika Zaidi
Tumejitolea kutii miongozo mipya zaidi ya WCAG kwa kiwango bora kadri tuwezavyo ili kuhakikisha kwamba maudhui yetu yanapatikana iwapo unatembelea Kitovu cha Kimataifa cha Raslimali kupitia njia ya kuona, kugusa au kuzungumza.
Hata hivyo, ni muhimu pia kutambua kwamba mfumo wa uendeshaji wa kompyuta yako na kivinjari chako cha mtandao pia una vipengele vya ufikiaji vilivyojengewa ndani ambavyo unaweza kuvitumia. Kwa kubadilisha mipangilio kwenye kifaa chako, inamaanisha kwamba upendeleo wako umehifadhiwa. Hivyo, tovuti yoyote unayotembelea itarekebisha kiotomatiki kulingana na mipangilio yako ya ufikiaji iliyohifadhiwa.
Mifano ya kawaida ya marekebisho hayo ni pamoja na kubadilisha mipangilio yako ili iweze kukusaidia vitu kama ubadilishaji wa rangi na uongezaji wa ukubwa wa maandishi. Hapa kuna mwongozo wa namna ya kufanya hivyo. Tafadhali zingatia kwamba mwongozo huu unaweza kutofautiana kulingana na kifaa na toleo la mfumo wa programu unayotumia.
Jinsi ya kufanya maandishi kuwa makubwa zaidi
Katika Kompyuta:
- Bonyeza Ctrl + Plus (+) ili kufanya maandishi kuwa makubwa zaidi.
- Bonyeza Ctrl + Minus (-) ili kufanya maandishi kuwa madogo.
- Bonyeza Ctrl + 0 ili kuweka upya ukubwa.
- Kwenye Mac, tumia Cmd badala ya Ctrl.
- Au nenda kwenye Mipangilio ya kivinjari chako na utafute “Kuza” au “Ukubwa wa herufi.”
- Kwenye Mac yako:
Kwenye Mac yako, chagua menyu ya Apple > Mipangilio ya Mfumo, kisha ubofye Ufikiaji kwenye ukingo pembeni.
- Bofya Onyesho, sogeza chini hadi Maandishi, kisha ubofye “Ukubwa wa maandishi.”
- Vuta slaida kulia ili kuongeza ukubwa wa maandishi kwenye deskitopu, katika ufito wa pembeni wa programu, na katika programu zilizoorodheshwa (ikiwa zimetengenezwa kutumia ukubwa wa usomaji unaopendelewa).
- Kwenye iPhone (Safari): Nenda kwenye Mipangilio > Programu > Safari > Kuza Ukurasa na uchague ukubwa.
- Kwenye Android (Chrome): Gusa doti tatu (juu kulia), nenda kwenye Mipangilio > Ufikiaji, na sogeza slaida ya kuongeza maandishi.
Tazama njia zingine za kubinafsisha Muhtasari wako wa Ufikiaji katika Android.
Jinsi ya Kubadilisha Rangi kwa Ajili ya Utofautishaji Bora
Windo:
- Tumia zana za bure kama vile Daki rida au lizadi ya midinaiti.
- Nenda kwenye Mipangilio> Ufikiaji> Tofautisha Mandhari ili kubadilisha rangi.
- Bonyeza Alt + Left Shift + PrintScreen ili kuwasha/kuzima utofautishaji wa juu.
Mac (Safari):
- Jaribu Njia ya Dark Nightshift (bila malipo).
- Bonyeza Cmd + Alt + Ctrl + 8 ili kubadilisha rangi
iPhone:
- Nenda kwenye Mipangilio > Ufikiaji > Onyesha & Ukubwa wa Maandishi.
- Washa Ongeza Utofautishaji au kigeuzi cha haraka.
- Ili kufanya mabadiliko kwa haraka, nenda kwenye Njia ya Mkato ya Ufikiaji na uweke mipangilio ya ufikiaji wa haraka.
Chromebook (Kivinjari cha Chrome): Bofya Ctrl + Search + H ili kubadili rangi):
Android (Chaguo hutegemea na kifaa):
- Samsung: Nenda kwenye Mipangilio> Ufikiaji> Uboreshaji wa Mwonekano> Ubadilishaji wa Rangi au Mipangilio> Mandhari>Chagua mandhari
- Google Pixel: Nenda kwenye Mipangilio > Ufikiaji > Rangi & Mwendo > Ubadilishaji wa Rangi.
- Tableti: Nenda kwenye Mipangilio > Ufikiaji > Ubadilishaji wa Rangi.
Chromebook (Kivinjari cha Chrome): Bonyeza Ctrl + Search + H ili kubadilisha rangi.
Kuna njia nyingine nyingi za kuboresha ufikiaji kupitia kivinjari chako, mfumo wa uendeshaji na kompyuta yako, simu janja au tableti. Tazama ukurasa wetu wa maelezo kuhusu programu za simu zinazoweza kukusaidia kuendelea kuboresha matumizi yako ya mtandaoni.
Vipengele vingine Muhimu vya ufikiaji
Android na Chromebook
Vipengele muhimu vya ufikiaji wa Android
Vipengele muhimu vya ufikiaji vya Chromebook
IOS – App (Programu ya IOS)
Vipengele muhimu vya ufikiaji kwa ajili ya kusikia
Vipengele muhimu vya ufikiaji kwa ajili ya Kuona
Vipengele muhimu vya ufikiaji kwa ajili ya kunena
Vipengele muhimu vya ufikiaji kwa ajili ya ujongevu
Vipengele muhimu vya Ufikiaji wa Kivinjari
Vivinjari vingi vina zana saidizi za ziada. Bofya kwenye viungo vya baadhi ya zana maarufu ili kufahamu kuhusu vipengele vyake muhimu vya ufikiaji:
Soma taarifa yetu ya ufikivu hapa