Je, hii inamfaa nani?

Walimu

Mwaka wa kuchapishwa
April 2026
Imetengenezwa na
National Resource Centre on Deafblindness- NRCDB, CDD.

Katika hali nyingi, mara nyingi, wazazi na walimu hukabiliwa na changamoto wanapowajumuisha watoto wenye ulemavu wa Uziwikutoona katika shule za kawaida. Huenda wasitambue namna bora ya kuwasaidia wanafunzi hawa wanapokuwa darasani. Hivyo, rasilimali hii itawasaidia kuelewa mambo gani wanapaswa kufanya ili kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa uziwi kuzoea na kujifunza vyema.

  • Toa mafunzo kwa wanafunzi wenye Uziwikutoona kuhusu darasa na maeneo mengine kama vile maktaba, choo n.k. ili waweze kujua eneo lao.
  • Panga vifaa vyote vya darasani katika maeneo maalum. Zitambulishe kila samani na nafasi zake ili waweze kukifkia kila kitu kwa urahisi.
  • Hakikisha kwamba, darasani kuna mwanga wa kutosha na punguza kelele zinazotoka nyuma.
  • Hakikisha kwamba wanafunzi wenye ulemavu wa Uziwikutoona wanakaa kwenye viti/safu ya mbele. Itakuwa ni rahisi kwa mwalimu kutangamana nao. Mwalimu atapaswa kuzungumza kwa sauti ya juu kidogo na kuandika maandishi makubwa ubaoni.
  • Tumia vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na vitu vya mfano pale inapowezekana.
  • Tambua njia ya mawasiliano anayoipendelea mwanafunzi (lugha ya ishara, lugha ya maneno na ya kugusa) na uwasiliane naye kwa kutumia njia hiyo
  • Waonyeshe wanafunzi wengine jinsi gani wanaweza kuwasaidia wanafunzi wenzao wenye ulemavu wa Uziwikutoona.
  • Andaa mikutano ya mara kwa mara na wazazi wao kuhusu maendeleo ya mtoto wao.

Pakua

Je, hii ilifaa

Maelezo haya yamekusaidia?

Changia


Raslimali zinazofanana

Mchezo Wa Mjongeo Na Hisia Kwa Watoto Wenye Uziwikutoona: Seti Ya Zana Kwa Mtoa Huduma

Rasilimali hii inatoa mwongozo hatua kwa hatua kuhusu kutumia michezo na shughuli za mwendo—kama vile kuzungusha, bakuli za hisia, na michezo ya mpira—kusaidia maendeleo ya mwili, hisia, na kijamii kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuona.

Muziki Na Mjongeo Kwa Watoto Wenye Uziwiupofu: Mwongozo Wa Vitendo

Mwongozo huu unatoa njia za vitendo kwa walei na walimu kutumia muziki na mwendo kusaidia kujifunza, mawasiliano, na ujumuishaji kwa watoto wenye ukosefu wa kuona na kusikia.

Hadithi ya mwalimu Adrian Maula

Adrian Maula ni mwalimu katika Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, akieleza umuhimu wa Global Deafblindess Resource Hub katika kutoa vifaa vya kufundisha na elimu tangu kuanzishwa kwa kituo hicho. “Naitwa Adrian Maula ni mwalimu wa kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu hapa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko. Siku yangu hapa shuleni…