Kitovu cha Kimataifa cha Raslimali za Uziwikutoona Duniani kimeundwa na Sense International. Sisi ni shirika la hisani linaloongoza kutoa misaada ili kuwasaidia watu wenye ulemavu wa Uziwikutoona katika nchi nane ulimwenguni.
Uzoefu Wetu
Tuna uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika kuwasaidia watu wenye ulemavu wa uziwikutoona kutambua haki zao. Kazi yetu ilianza mnamo mwaka 1994 ikiwa na lengo la kubadilishana maarifa na utaalamu wa shirika letu mama, la Sense UK.
Tangu wakati huu, tumeanzisha mashirika ya ndani ambayo yamesajiliwa katika nchi za India, Kenya, Peru, Romania, Tanzania na Uganda. Pia tumeanzisha programu za kazi kwa ushirikiano na mashirika ya kitaifa nchini Bangladesh na Nepal.
Tafuta ofisi ya Sense International iliyo karibu nawe
Kazi zetu
Tunafanya kazi ya kutambua watoto walio na uziwikutoona mapema iwezekanavyo katika kipindi cha awali cha maisha yao, ili kwa kuwapatia usaidizi stahiki, waweze kustawi. Pia tunaboresha upatikanaji wa elimu bora na mafunzo ya ufundi stadi ili watoto na vijana wenye Uziwikutoona waweze kujitegemea, kuanzisha maisha na kutimiza uwezo wao kamili.
Kazi yetu inatumia mbinu ambazo huzingatia haki. Tunawasaidia watu wenye ulemavu wa uziwikutoona na familia zao kupinga unyanyapaa, ubaguzi na vikwazo vingine vilivyopo ndani ya jamii ili haki zao zitambuliwe na kupatikana – kwa sasa na katika siku zijazo.
Tembelea tovuti yetu ili kujua zaidi kuhusu maono, dhamira na kazi zetu
Kitovu cha Kimataifa cha Raslimali za Uziwiupofu uziwikutoona Duniani
Kitovu cha Kimataifa cha Rasilimali za Uziwikutoona Duniani ni jukwaa la mtandaoni ambalo huwapa watu wenye Uziwikutoona na wale wanaowaunga mkono, uwezo wa kupata taarifa, maudhui na rasilimali zinazoweza kupatikana.
Kitovu ni zana muhimu ya teknolojia ambayo inalenga kusaidia kukamilisha na kuimarisha kazi tunayofanya katika nchi nane tunazofanyia kazi. Lengo kuu la Kitovu cha Kimataifa cha Raslimali za Uziwikutoona Duniani ni kwamba linatumika kama jukwaa la kidijitali ambalo linawawezesha watu wenye ulemavu wa Uziwikutoona/Ulemavu Mchanganyiko kupata taarifa, rasilimali na maudhui kwa namna iliyo sawa na watu wasio na ulemavu na kujifunza kuhusu ulimwengu unaowazunguka.
Peruzi rasilimali zetu