Iwe unafikia Kitovu cha Kimataifa cha raslimali za Uziwikutoona Duniani kupitia kuona, kugusa au kuzungumza, tunataka kazi hii ifanyike vizuri zaidi kwa ajili yako kadri iwezekanavyo.

Ahadi yetu

Tumejitolea kutii Miongozo ya Ufikiaji wa Maudhui ya Wavuti (WCAG) kiwango cha AA.

Tovuti yetu inapaswa kuendana na visoma skrini vya kisasa na programu ya utambuzi wa usemi. Inapaswa kuitikia ipasavyo vikuza, mandhari ya utofautishaji wa hali ya juu na zana za hotuba ambazo zimeundwa katika mifumo ya uendeshaji ya kisasa.

Mfumo wa AbilityNet unatoa mwongozo wa jinsi ya kufanya tovuti zikufae wewe pamoja na mahitaji yako.

Mfumo wa NV Access unakupa programu ya kupakua ya bure ya kusomea skrini.

Tunajitahidi kujaribu tovuti yetu kwa kutumia teknolojia mbalimbali, lakini hatuwezi kujitolea kujaribu kila toleo la kivinjari kwa kila toleo la teknolojia ya usaidizi, wala kufanya majaribio kwenye kila toleo la mfumo wa uendeshaji au kila aina ya simu ya mkononi.

Kukifanya kivinjari chako kiweza kufikiwa

Kuna vipengele vya ufikivu vilivyoongezwa ambavyo vinapatikana katika vivinjari mbalimbali navyo ni kama vifuatavyo:

Tovuti za watu wengine

Katika baadhi ya maeneo kwenye tovuti yetu, tunashiria au kukuelekeza katika tovuti za watu wengine na programu ambazo hutoa taarifa muhimu na ushauri kwa watumiaji wetu. Hta hivyo, hatuwezi kuthibitisha kwamba tovuti na programu hizi za washirika wengine zinapatikana kikamilifu na zinatii miongozo ya WCAG. Pale inapowezekana tunajitahidi kushirikiana na wahusika hawa kufanya mabadiliko yanayohitajika ili kuendana na miongozo ya WCAG na kuboresha ufikiaji wao.

Je, tunaendeleaje?

Tunafanya kila juhudi ili maudhui yote kwenye tovuti yetu yaweze kufikiwa lakini kuna uwezekano kwamba baadhi ya maeneo ya tovuti yetu bado yanahitaji maboresho katika eneo hili. Tunafanya kazi kwa juhudi ili kuboresha ufikivu wetu na matumizi ya mtumiaji na kuendelea kupokea mrejesho kutoka kwa watumiaji ili kutusaidia kuboresha hili. Ikiwa una matatizo ya kufikia tovuti yetu, tafadhali wasiliana nasi.