Je, hii inamfaa nani?

Waalimu, Wanafunzi , Wazazi, Watunga sera & Wasimamizi

Mwaka wa kuchapishwa
July 2025
Imetengenezwa na
Sense International Tanzania

Agness ni msichana mdogo anayesoma elimu ya msingi. Ndoto yake ya kupata elimu ilikaribia kufa kabla ya kukutana na Sense International waliomsaidia kwa vifaa vya kutembea (kitimwendo) na kubadilisha maisha yake.

Maelekezo elekezi ya video ya Agnes

  Msimuliaji: 

Karibu kwenye “: Safari ya Elimu Jumuishi.ya Agness”, Njia hii ya kuielekea elimu jumuishi ni muhimu ingawa ina changamoto nyingi sana hasa kwa mtoto mwenye ulemvu. Leo, tunamlenga Agness, mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo, ambaye maisha yake ya kielimu yamebadilika kupitia kushiriki kwake kwenye Mradi wa Task Order 51 (TO51). Mradi ambao unalenga kuwezesha mtoto mwenye ulemavu kupata elimu bora kwenye darasa jumuishi ikienda sambamba na zoezi la ubainishaji na upimaji wa mahitaji ya kielimu kwa watoto wenye ulemavu na utoaji wa afua stahiki kwa kila mtoto. Mradi wa TO51 unalenga kuboresha hali ya elimu kwa watoto wenye ulemavu. Hadithi ya Agness inadhihirisha jinsi upimaji na utolewaji wa afua stahiki kwa mtoto mwenye ulemavu unavyoweza kuunda mazingira jumuishi ambapo kila mtoto anaweza kufanikisha hatua nyingi na kufikia ndoto zake. Kwa kuzingatia mahitaji ya kila mtoto mwenye ulemavu tunaweza Saidia na kuruhusu kila mtoto kufikia kile anachokiweza. Kutana na Agness, mwanafunzi mahiri, ambaye safari yake ya elimu imetolewa kikazwo kikubwa kwa kupatiwa kitimwendo , Tangu apatiwe kitimwendo Agness amekua mhudhuriaji mzuri wa shule kwa sasa, ushirikano na wanafunzi wenzake umeimarika. Hapa mama yake anaelezea jinsi kitimwendo alichopatiwa Agness kimebadilisha maisha ya Agness shuleni , na kumuwezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za shule na kuunda urafiki na wanafunzi wenzake. 

Maelezo picha: 

 Shule inaonekana kwa juu 

Agness anacheza na rafiki yake darasani huku akifurahi, amekaa kwenye kitimwendo na rafiki yake amekaa kwenye dawati. 

Agness amekaa kwenye kitimwendo chake anasukumwa na rafiki yake kuelekea darasani. 

Matairi ya kitimwendo cha Agness yanapada kueingia darasani. 

Agness anaingia darasani akisukumwa kwenye kitimwendo chake. 

Daktari wa macho anapima uoni wa mtoto kwa kumuonyesha herufi zilizo kwenye karatasi ukutani. 

Mwalimu anawasimami wanafunzi darasani kujifunza na kuandika. 

Agness yupo darasani pamoja na wanafunzi wanzake huku akiandika kwenye daftari lake. 

Mwalimu anawasimamia wanafunzi wake darasani. 

Mtoto mweye ulemavu wa utindio wa ubongo akifanyiwa majaribio ya kitabibu na daktari. 

Agness amekaa darasa ananyoosha kidole, anashika kipaza sauti anajibu swali. 

Marafiki zake Agness wanamsukuma akiwa amekaa kwenye kitimwendo wakienda shule. 

Marafiki zake Agness wanamsukuma Agness kwa nyuma kwenye kitimwendo wakiingia eneo la shule. 

Mama Agness 

Kumpeleka shuleni nilikuwa nikimbeba mgongoni lakini kazi zikiwa zimenizidi haohao rafiki zake ndio walikuwa wanambeba na kumrudisha wenyewe. Mradi ulipotupa haka kabaiskeli kamwendokasi hapo ndipo tulipoona unafuu na Agness ndipo alipozidi kuipenda shule akajua na kusoma maana kipindi cha kwanza mpaka wamekuja kufunga muhula wa mwisho alikuwa anajua kusoma kidogo, sasa alipoletewa kile kibaiskeli ndio kamampa changamoto kwamba kumbe nisome na mimi ni mtoto kama wengine. Na wanafunzi ndipo walipompenda na walimu pia, Agness anajua kusoma. 

Maelezo picha: 

Mama Agness amekaa kwenye kiti anaongea kuhusu Agness. 

Mama Agness amembeba Agness anampeleka shule. 

Mama Agness amekaa kwenye kiti anaongea kuhusu Agness. 

Agness amekaa darasani anaandika kwenye daftari. 

Mama Agness amekaa kwenye kiti anaongea kuhusu Agness. 

Msimuliaji: 

Mradi wa TO51 umekua mstari wa mbele katika kutoa msaada na usaidizi wa watoto wenye ulemavu, ikiwa ni pamoja na huduma ya ubainishaji na upimaji wa mahitaji ya ujifunzaji, huku ikishauri na kupendekeza afua stahiki kwa kila mtoto kulingana na mahitaji yake, walimu na wadau wa sekta ya elimu wamepatiwa mafunzo kwa namna bora ya kuwabaini, kuwapima na kuwasaidia watoto wenye ulemavu ili kuboresha ujifunzaji kama ilivyofanyika kwa Agness. Agness ni miongoni mwa watoto zaidi ya 500 ambao mradi kupitia kituo cha upimaji MITINDO – Misungwi kiliwabainisha na kuwapima kufahamu mahitaji yao ya kielimu, Agness alibainishwa na kuletwa kupimwa na baada ya kupimwa wataalamu walishauri Agness kupatiwa kitimwendo lakini pia baadhi ya mapendekezo yalielekezwa shuleni kwa namba bora ya kusaidia safari ya ujifuzaji na ujifundishaji ya Agness. 

Maelezo picha: 

Kamera inasogea kutoka jengo la upimaji kuonyesha mazingira ya juu ya kituo. 

Mtaalamu wa upimaji anaandika majibu ya vipimo mwanafunzi. 

Mwalimu amesimama mbele ya darasa anafungua madaftari, wanafunzi wamekaa kwenye madawati wanaangalia ubaoni. 

Mtaalamu wa upimaji anamuonyesha vidole mtoto kwa ajili ya kupima uoni. 

Mtoto anasimama juu ya mzani kupima uzito. 

Agness anapandishwa kwenye kiti mwendo na wanafunzi wenzake tayari kwa kwenda shule. 

Agness anasukumwa kwenye kiti mwendo na rafiki zake kwenda shule. 

Mtaalamu wa vipimo: 

Katika kituo cha upimaji tunapima mtoto mwenye uhitaji maalumu ili tuwezekujua changamoto aliyonayo katika ujifunzaji. Na kwa nini tunataka kujua? Tunataka kujua kwa sababu inatusaidia kushauri shule gani inafaa kwa ajili ya huyu mtoto aweze kupata elimu, kushari walimu ni namna gani mtoto huyo anaweza kufundishwa, mahali gani akae darasani wakati wa kujifunza, lakini pia tunambaini ni hitaji gani hasa linahitaji kwa mtoto. Kwa mfano mtoto anawezakuja kumbe ili aweze kupata elimu vizuri anahitaji apate vifaa saidizi. Kwa hiyo tunashauri kifaa zaidizi ambacho kinafaa kumsaidia mtoto. 

Maelezo picha: 

Mtaalamu wa vipimo amekaa kwenye kiti na meza anaongea. 

Mtaalamu wa vipimo anaandika taarifa za vipomo huku mama wa mtoto anasubiri majibu. 

Mtoto anafanyiwa vipimo kwa njia ya mchezo wa kupanga maduara ya plastiki. 

Mtaalamu wa vipimo amekaa kwenye kiti na meza anaongea. 

Msimuliaji 

Kutokana na ubaguzi na unyanyapaa hasa kwa watu wenye ulemavu , bado safari ya Agness ilikua ngumu kiasi kuweza kuwa shuleni, hasa kwa siku za mwanzo. 

Maelezo picha 

Agness amekaa darasani anaandika kwenye daftari lake la mazoezi. 

Mama Agness 

Kipindi anaanza shule maisha yake yalikuwa magumu sana, maana kipindi tu nilipompeleka shuleni siku ya kumuandikisha nikamuacha shuleni wakati namfuata kurudi nyumbani ndio akawa ananiambia njiani, “mama wanafunzi wananishangaa wananizingira halafu wanaambiza kakilema.” Hapo ndio nikawa namtia moyo “hapana mwanangu soma tu, wakikuzingira wakikwambia wewe ni kilema waambie sio wewe ni mipango ya Mungu, sawa? Anasema sawa. Lakini ukimpeleka shuleni wenzake ndio wanakuja wanasema, “mama, Agness shuleni alikuwa analia” alikuwa analilia nini? “Watu wakimuangalia analia, anasema eti wanamuangalia sana.” Nikawa namtia moyo hivyohivyo na ushirikiano wa walimu hivyohivyo wakawa wanambembeleza mwishowe akawa amezoeazoea. 

Maelezo picha. 

Mama Agness amekaa kwenye kiti anaongea mbele ya kamera. 

Mama Agness anamvalisha shati Agnes tayari kwa kwenda shule. 

Mama Agness anamuweka vizuri Agness kola ya shati tayari kwa kwenda shule. 

Mama Agness anamvalisha sweta Agness. 

Mama Agness amekaa kwenye kiti anaongea mbele ya kamera. 

Msimuliaji 

Ikilitambua hili, mradi ya TO51 kupitia shughuli zake ulifanikisha uanzishwaji wa klabu jumuishi za watoto mashuleni, ambazo zilikua zinahubiri Habari ya ujumuishi kwa wote, Agness akiwa ni miongoni wa wanafunzi wanaoshiriki kwenye klabu hizi ambazo watoto wanajifunza kupitia michezo na dhana mbalimbali za ujumuishi, Hii imesaidia kusambaza ujumbe wa kuwatambua na kuwathamini watu wote hasa wenye ulemavu, Mahudhurio ya Agness shuleni yamekua bora sana toka apatiwe kitimwendo, wakati maendeleo yake darasani pia yakiwa ni yenye kuridhisha kwa kiwango kikubwa. 

Maelezo picha 

Klabu ya wanafunzi wamekaa kwenye duara wanaimba huku Agness amekaa na kiti mwendo katikati ya duara. 

Klabu ya watoto wanazungumza darasani kwa kupokelezana kipaza sauti. 

Agness anashika kipaza sauti anaongea. 

Mwalimu anamuelekeza Agness kufanya kazi ya darasani. 

Baba Agness Anaongea 

Baada ya kuletewa hiki kitimwendo tuseme tu mahudhurio ya kwenda shule ya mtoto huyu ni ya hali ya juu, haijawahi kutokea ashndwe kwenda shule akiwa na hii baiskeli lakini sasa ikitokea hivyo labda awe na matatizo ya kiafya. 

Maelezo picha 

Baba Agness amekaa kwenye kiti anaongea nyuma yake kuna mazingira ya miti mingi. 

Picha ya juu ya shule inaonyesha mazingira ya shule. 

Mwalimu wa Agness. 

Jinsi mlivyomsaidia kupata kitimwendo, kwanza kumemuhamasisha kuja shule, haogopi, haoni aibu, amepata marafiki wengi na yeye anapenda kujifunza nao na kuwasaidia wao. Kwa hiyo kwenye upande wa mahudhurio Agness yupo vizuri labda tu kwenye changamoto kama kuumwa. Maendeleo yake kimasomo kwa kweli anapiga hatu nzuri kwa sababu anawazidi hata wale ambao hawana zile changamoto za kiafya. Anajitahidi ni mwanafunzi anayependa kujifunza kwa bidii, kuuliz maswali na huwa huwa anapenda aelewe na kwenye tatizo huwa anapenda kuuliza ili aelewe zaidi. Upande wa maendeleo yake yupo vizuri hata ukiangalia kwenye majaribio ya mitihani kwa mfano mitihaniya upimaji yupo vizuri. 

Maelezo picha: 

Mwalimu wa Agness amekaa kwenye kiti anaongea kuhusu Agness. 

Agness akiwa amezungukwa na marafiki zake huku wanasoma kitabu. 

Mwalimu wake Agness amekaa kwenye kiti anazungumza kuhusu maendeleo yake. 

Agness anaandika kwenye daftari lake na mitihani wake unaonekana. 

Agness anaandika kwenye daftari lake la darasani. 

Mwalimu wa Agness amekaa kwenye kiti anaongea kuhusu Agness. 

Agness anaandika kwenye daftari lake na mitihani wake unaonekana. 

Msimuliaji 

Maendeleo mazuri ya Agness hayajawa kwenye elimu yake tu, Bali mabadiliko ya namna anajumuishwa na wenzake, uwepo wa kitimwendo umebadilisha vingi kwenye maisha ya Agness, Bado Mama ake Agness anaikumbuka kwa furaha siku ambayo mwanae mpendwa alimfuata na kumweleza yafuatayo. 

Maelezo picha 

Agness anaonekana kwa mgongo yupo darasani. 

Agness anacheza na rafiki yake darasani huku wote wanacheka kwa pamoja. 

Mama Agness 

Kuna siku moja aliniambia hivi,”Mama na mimi siku hizi nafurahi kwa sababu naenda kusali mpaka Mabuki, wanasikuma hadi Mabuki, nilikuwa sijawahi kuliona kanisa la Mabuki, nakuja tu hivyo hivyo mdogo mdogo mama. Ukikutana na watu wengine njiani wanakupenda wanasimamisha gari wanakupa hela”. Na siku nyingine kweli huwa anarudi na vihela amepewa. Hilo mimi ndio nasukuru la kibaiskeli kwa sababu imemuwezesha kujua mazingira mbalimbali. Wakitaka kwenda kucheza wanamuweka tofauti na mgongoni maana siku nyingine walikuwa wanamuacha wanaona ni usumbufu wenzie wanamkimbia. Lakini sasa hivi wakitaka kwenda wanambeba Agness wanaenda. Wanamuweka kwenye baiskeli yake wanamsukuma wanaenda. Yaani hicho ndicho nilichoshukuru. 

Maelezo picha 

Mama Agnes amekaa kwenye kiti anazungumza. 

Msimuliaji 

Hadithi hii ya Agness ni Ushahidi tosha ya nguvu ya elimu jumuishi, Kuwa na mifumo bora ya ubainishaji na upimaji wa mahitaji ya ujifunzaji wa watoto wenye ulemavu, utoaji wa vifaa saidizi inawezekana kabisa kuunda mazingira bora ya elimu ambapo kila mtoto ana fursa ya kufanikiwa. Ili kuendelea kusaidia watoto wenye ulemavu, Mradi wa TO51 unahimiza mafunzo ya kina kwa wadau wa sekta ya elimu, programu za uhamasishaji na ubainishaji wa watoto wenye mahitaji , na upimaji wa mara kwa mara kwa watoto wanaobainishwa ili kutambua mahitaji yao ya kutoa afua stahiki . Ikiwa bado kuna wazazi wanaendelea kuficha watoto wenye ulemavu na kuwabakisha nyumbani hadithi ya Agness ni kielelezo tosha cha namna gani watoto wenye ulemavu wanavyoweza, Mradi umewezesha ujenzi wa kituo cha upimaji chenye lengo ya kusaidia upimaji endelevu kwa watoto kama ambavyo inahimizwa na kiongozi wa serikali. 

Maelezo picha 

Agness anasukumwa kwenye kitimwendo akiwa na rafiki zake wanaenda shule. 

Mazingira ya ndani ya darasa yanaonekana kwa juu, wanafunzi wamekaa darasani wanasoma. 

Mwalimu anawasimamia wanafunzi wafanye kazi za darasani. 

Mwalimu anaonekana mbele ya darasa akiwasaidia wanafunzi jambo la kitaaluma. 

Kituo cha upimaji kinaonekana kutoka juu kuonyesha mazingira ya ndani ya chumba cha upimaji. 

Kiongozi wa serikali 

Kwa kweli nitoe wito kwa wazazi, wazazi wawalete watoto kwenye kituo cha upimaji. Huko nyuma hatukuwa na kituo hicho na baada ya mradi kufika kwa neema ya Mungu tulibahitika kupata kituo hicho na hivyo kituo kimesaidia sana kutambua kiwango cha watoto katika kujifunza kwao. Lakini pia na namna ya kuweza kuwasaidia, kuna wengine ambao wanachangamoto za ugonjwa tunawaandikia rufaa na wanakwenda na hatimae wanapata matibabu na wanakuwa katika hali ambayo inahitajika. Kwa hiyo mimi niombe wazazi wasiache kuwaleta watoto, pale watapata ushauri upo ushauri wa kitaalamu lakini pia upo ushauri wa kidaktari lakini pia zipo hatua ambazo wanaweza wakasaidiwa. 

Maelezo picha 

Kiongozi wa serikali amekaa ofisini kwake anazungumza. 

Tangazo la Sense International Tanzania linaonekana kisha anaonekana mtaalamu wa vipimo vya watoto kisha mtoto anayefanyiwa vipimo. 

Kiongozi wa serikali amekaa ofisini kwake anazungumza. 

Msimuliaji 

Safari ya kutekeleza elimu jumuishi inaendelea, na kwa pamoja tunaweza kutengeneza siku za mwangaza kwa watoto wenye ulemavu na kupata haki ya elimu kama watoto wengine Makala hii fupi imeletwa kwenu na Mradi wa Task Order 51 unaotelekezwa na mashirika ya Sense International Tanzania, ADD International, Tanzania Cheshire Foundation na Light For the World katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga chini ya ufadhili wa Ofisi ya Mambo ya nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo – Uingereza 

Maelezo picha 

Klabu ya watoto inaonekana kutoka juu wakiwa wanaimba na kupiga makofi, shule pia inaonekana kutoka juu huku mazingira ya miti mingi. 

Shule inaonekana kwa kuzungukwa na kamera kutoka juu. 

Chapa za nembo ya taifa la Tanzania, Add International, Tanzania Chesire Foundation, Light for the World, Inclusive Futures na Sense International Tanzania zinaonekana kwenye skrini.  

Je, hii ilifaa

Maelezo haya yamekusaidia?Inahitajika
This field is for validation purposes and should be left unchanged.

Changia


Raslimali zinazofanana

Watoto wanaoishi na uziwikutoona

Shughuli za kila siku za watoto wanaoishi na uziwikutoona.

Festo – Kijana mwenye uziwikutoona, Tanzania

Video ya kijana mwenye uziwikutoona akijiingizia kipato kwa kufanya shughuli ya utengenezaji wa vikapu.

Philbert – Kijana mwenye uziwikutoona kutoka Tanzania

Ujumuishaji wa vijana wenye uziwikutoona kwenye shughuli za kiuchumi.