Je, hii inamfaa nani?

• Waalimu
• Wanafunzi
• Wazazi
• Watunga sera
• Wasimamizi

Mwaka wa kuchapishwa
February 2026
Imetengenezwa na
Sense International Tanzania

Adrian Maula ni mwalimu katika Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, akieleza umuhimu wa Global Deafblindess Resource Hub katika kutoa vifaa vya kufundisha na elimu tangu kuanzishwa kwa kituo hicho.

“Naitwa Adrian Maula ni mwalimu wa kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu hapa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko. Siku yangu hapa shuleni huanza kwa kukagua majukumu yangu niliyonayo kwa siku husika na kuhakikisha kila kitu kipo kwenye nafasi yake na huendelea kadri majukumu ya siku hiyo yanavyokuwa.

Kwa mara ya kwanza nilisikia kuhusu Global Deafblindness Resource Hub ilikuwa Dodoma kwenye uzinduzi wa wa kituo hicho na kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kukitumia kitovu wakati wa uzinduzi wake.

Napenda kusoma muongozo wa ufundishaji wa wanafunzi wenye uziwikutoona, kwa mimi mwalimu ile ndio sehemu ambayo napenda zaidi kutembelea kwa sababu inanisadia kwenye ufundishaji na hiyo ndio rasilimali ambayo ni muhimu zaidi kati ya zote zilizopo kwenye Kitovu cha Kimataifa cha rasilimali za uziwikutoona.

Adrian akitazama Global Deafblindness Resource Hub kwenye simu yake.
Adrian akitazama Global Deafblindness Resource Hub kwenye simu yake.

Niliwahi siku moja kusahau kitabu cha muongozo wa mwanafunzi nyumbani, Global Deafblindness Resoruce Hub ilinisaidia sana kwa sababu badala yake nilitumia tu mtandao huo na kufungua kitabu mtandaoni na kuendelea na majukumu mengine.

The Global Deafblindness Resource Hub inafikika kirahisi sana, sijawahi kuwa na changamoto ya kuitumia kwa sababu namna ilivyowekwa ni nyepesi sana kuweza kufikika. Kwa sasa kwa kuwa bado Hub inaendelea kuwekwa rasilimali bado hakujawa na rasilimali nyingi ambazo naweza nikazitumia darasani moja kwa moja, nyingi ni kwa ajili kuongeza ujuzi tu kuhusu uziwikutoona.

Maendeleo ya teknolojia yanaenda yanaongezeka siku za mbeleni kila kitu tunachotumia kama nyezo ya kufundishia nakiona kikienda kuwa mtandaoni na Global Deafblindness Resource Hub ni mwanzo mzuri wa kuelekea safari hiyo. Napenda kuona siku moja Global Deafblindness Resource Hub imejaa rasilimali zote ambazo tunazo kwenye mifumo ya vitabu.”

Adrian aliketi darasani mwake akitazama simu yake.
Adrian aliketi darasani mwake akitazama simu yake.

Je, hii ilifaa

Maelezo haya yamekusaidia?

Changia


Raslimali zinazofanana

Mchezo Wa Mjongeo Na Hisia Kwa Watoto Wenye Uziwikutoona: Seti Ya Zana Kwa Mtoa Huduma

Rasilimali hii inatoa mwongozo hatua kwa hatua kuhusu kutumia michezo na shughuli za mwendo—kama vile kuzungusha, bakuli za hisia, na michezo ya mpira—kusaidia maendeleo ya mwili, hisia, na kijamii kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuona.

Marekebisho ya Darasa kwa Ajili ya Wanafunzi Wenye Uziwikutoona

Rasilimali hii inatoa mwongozo juu ya jinsi ya kufanya marekebisho ya darasani kwa watoto wenye ukosefu wa macho na kusikia.

Muziki Na Mjongeo Kwa Watoto Wenye Uziwikutoona: Mwongozo Wa Vitendo

Mwongozo huu unatoa njia za vitendo kwa walei na walimu kutumia muziki na mwendo kusaidia kujifunza, mawasiliano, na ujumuishaji kwa watoto wenye ukosefu wa kuona na kusikia.