Je, hii inamfaa nani?
Waalimu, Wanafunzi, Wazazi, Watunga sera na Wasimamizi
Festo ni kijana mwenye uziwikutoona, anatumia ujuzi wake wa kutengeneza vikapu kujiingizia kipato na kuwa hamasa kwa vijana wengine wenye uziwikutoona.
Maelekezo elekezi ya video ya Festo
Maelezo picha
Chapa ya Community Fund inaonekana kulia na chapa ya Sense International kushoto.
Maneno ‘Festo Romwandi – Uziwikutoona’ yanatokea na kutoweka.
Maneno yanatokea ‘Festo Romwadi, kijana mwenye ulemavu wa uziwikutoona, ambaya anaishi Ifakara mkoani Morogoro, anajishughulisha na mradi wa kutengeneza vikapu kwa msaada aliopewa na mama yake’
Msimuliaji: Hapa tunakutana na kijana Festo Romwadi…Anawashangaza wengi kutokana na taalamu yake ya kushona vikapu vya aina mbalimbali… Sense International ndio wadhamini wa vijana wote hawa.
Maelezo picha
Festo anaonekana kwa karibu akishona vikapu, vikapu vinaonekana.
Festo amekaa kwenye kiti chini ya mti mbele ya vikapu anaongea na mtumishi wa Sense kwa lugha ya alama
Festo anashona vikapu
Festo kasimama mbele ya wana mama wakiwa wote wameshika vikapu vilivyotengenezwa na Festo
Picha mnato, Festo anatembea mbele ya mama yake wamshika vikapu mikononi. Picha mchanganyiko zikionyesha Festo akitengeneza vikapu.
Picha inasimama na maneno ‘Festo Romwadi’ yanatokea
Festo anatengeza vikapu huku nyuma yake watu kadhaa wakiwa wanamuangalia
Mama Festo: Jina langu ni Theresia Romwadi Mbarika. Mwaka 2000 nikapata ujauzito wa Festo nikajifungua katika hospitali ya Mtakatifu Francis, akiwa ni mlemavu wa macho hivyo hivyo hajaugua .
Maelezo picha:
Mama yake Festo amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yake akiongea
Kwa karibu Festo anaonekana anashona vikapu
Mama yake Festo amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yake akiongea
Mtumishi wa Sense anamuweka Festo kwenye kiti na kuanza kuongea nae kwa lugha ya alama.
Festo: Jina langu naitwa Festo, nashukuru Sense kwa kunisaidia, walinipa mtaji ambao uliniwezesha kuandaa hivi vikapu.
Maelezo picha:
Festo amekaa kwenye kiti pembeni yake yupo mtumishi wa Sense wanaongea kwa lugha ya alama
Mama Festo: Festo shule amesomea Iringa kuna shule pale ipo Kihesa, shule ya walemavu wasioona, bubu na viziwi. Mimi nilikuwa naenda kila baada ya likizo nampeleka shule ikifungwa naenda kumchukua narudi nae nyumbani.
Maelezo picha:
Festo amekaa kwenye kiti pembeni yake yupo mtumishi wa Sense wanaongea kwa lugha ya alama
Festo amekaa kwenye kiti pembeni yake yupo mtumishi wa Sense wanaongea kwa lugha ya alama
Shangazi yake Festo:Kwa mchango wangu wa kumsaidia mwanangu Festo nilikuwa sina cha kutafuta mwenyewe cha kusema nimkabidhi mwanangu nimsaidie hiki, Mungu mwenyewe atamsaidia. Mchango wangu mkubwa ulikuwa nikisikia kuna semina au kikao cha wototo masikini walemavu mimi nilikuwa nachukua baskeli nambeba mwanangu naangaika nae. Nikirudi nikisikia kesho wapi mimi naenda nae mpaka huku mjini kote nikawa nafika nae mwanangu Festo.
Maelezo picha:
Festo anaonekana uso wake kwa karibu akiwa anashona vikapu, anachukua mkasi anakata plastiki.
Shangazi yake Festo amekaa kwenye kiti huku amejifunika kikoi na akiongea
Festo amekaa kwenye mkeka pembeni yake amezungurukwa na vikapo na nyuma yake watu wakimtazama akiwa anatengeneza vikapu.
Festo anatoka ndani ya nyumba anatembea huku ameshika vikapu nyuma yake mama yake anamfuata huku ameshika vikapu mikononi
Shangazi yake Festo: Wanaume wengi wanawakimbia walemavu kwa sababu wanaona mtoto mlemavu ni kazi sana kumlea kwake na huduma zake ni nyingi. Kwa hiyo nifanyaje, wanaamua kuondoka mzigo nimuachie mama, na mama unashindwa kukimbia, je, nimuachie nani na Mungu kakupa?
Maelezo picha:
Shangazi yake Festo amekaa chini ya mti huku amejifunika kikoi akiongea
Festo amesimama mbele ya ndugu zake huku wameshika vikapu vilivyotengenezwa na Festo.
Mama Festo: Baada ya kumaliza hiyo miaka kumi kule shuleni yule mwalimu alikuja nyumbani nilipokuwa nakaa, akaniambia huyu kuna sehemu inatakiwa nimuunganishe, kuna pesa za wafadhili ambazo zinatoka kwa watu kama hawa, kwa hiyo leo kuna maswali nitakuuliza, baadae muda wowote na saa yoyote jina lake likitoka mtaitwa kwenda kwenye semina hapo mtajulishwa nini kitakachofanyika.
Maelezo picha:
Mama yake Festo amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yake akiongea
Festo anaandaa plastiki maalamu kwa ajili ya kushonea vikapu nyuma yake watu wakiwa wanamtazama.
Mama yake Festo amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yake akiongea
Kamera inamuonyesha Festo kwa karibu huku akiwa anashona vikapu, nyuma yake watu wakimtazama, anatumia mkasi kukata plastiki
Festo: Nimejifundisha Iringa na hapa sasa napambana mimi mwenyewe kwa ajili ya kujiendeleza.
Maelezo picha:
Kwa lugha ya alama Festo anazungumza na mtumishi wa Sense huku wakiwa wamekaa kwenye viti chini ya mti pembeni yake wakiwa na vikapu vya Festo.
Kamera inamuonyesha Festo kwa karibu akiwa anakata kwa mkasi plastiki nyuma yake wanamama watatu wanamuangalia kwa makini
Shangazi yake Festo: Lakini alivyoenda huko tunaona Mungu kambarikia mtoto anajua kusoma kwa ishara hata ukimuuliza jina lake anaandika.
Maelezo picha:
Shangazi yake Festo amekaa chini ya mti amejifunika kikoi akizungumza.
Festo anaongea kwa lugha ya alama na mtumishi wa Sense huku wote wakiwa wamekaa chini ya mti kwanye viti
Mama yake Festo amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yake akiongea
Mama Festo: Tukaenda Dar es Salaam tukapokelewa vizuri, tukala vizuri, tukalala pazuri. Tulikuwa kama 16 hivi, tulivyokaa siku nne kwenye semina wakatuambia kuwa kutakuwa na hela kidogo mwende mkawafungulie akaunti na kuanza miradi midogo midogo ya kuwasaidia hawa watoto.
Maelezo picha
Mama yake Festo amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yake akiongea
Kamera inamsogelea Festo ambaye amekaa chini ya mti anashona mikoba ya plastiki
Mama yake Festo amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yake akiongea
Shangazi yake Festo: Mpaka hivi amepata kazi yake, fani yake ya kushona vikapu vile, kuna vitu vingine pia vya kushona sasa vitendea kazi kapata kimoja.
Maelezo picha
Mikoba ya plastiki inaonekana kutoka juu, Festo amekaa pembeni yake akishona mikoba hiyo
Shangazi yake Festo amekaa chini anaongea
Festo: Ninachopenda watu wanisaidie ni kuendeleza biashara yangu au kuongezewa mtaji ili niweze kuandaa vikapu vingi zaidi.
Maelezo picha
Mtumishi wa Sense akiongea na Festo kwa lunga ya alama huku wamekaa chini ya mti mbele ya vikapu vya Festo
Festo amekaa chini na vikapu vyake anavyovitengeneza nyuma yake watu wanamuangalia akiwa anatengeneza vikapu.
Mwanaidi Kishwege: Sense iendelee kumuona Festo, iendelee kumsaidia zaidi kwa hapa alipo kwa sababu mpaka sasa hivi Festo anatengeneza vikapu hivyo lakini bado soko ni dogo.
Maelezo picha
Mwanamama amesimama anaongea
Festo: Hali ya masoko bado ni ngumu kidogo kwa kikapu kama hiki ni shilingi elfu nane na kikapu hiki ni shilingi elfu nne.
Maelezo picha
Mtoto mdogo anakatiza mbele ya Festo ambaye amekaa chini anasuka vikoba
Mtumishi wa Sense akiongea na Festo kwa lunga ya alama huku wamekaa chini ya mti mbele ya vikapu vya Festo
Festo anatengeneza vikapu kwa kutumia plastiki huku watu wakiwa wanamuangalia kwa nyuma
Festo anazungumza na mtu ambaye wote wamekaa chini huku wameshika vikapu
Mwanaidi Kishwege: Kwa sababu soko la hapa kijijini ni la rejareja, lakini kama Sense ikamsaidia kumuonyesha mwanga zaidi ingeweza kusaidia angalau soko linaloweza kumuuzia hizi bidhaa zake kwa wingi zaidi tofauti na ilivyokuwa sasa.
Maelezo picha
Wanamama wamesimama na Festo huku wote wameshika vikapu vya plastiki vilivyotengenezwa na Festo
Mwanamama amesimama mbele ya nyumba anazungumza.
Festo: Wakipenda kujifunza mimi nipo na nina uwezo wa kuwasaidia watu wengine ambao wangependa kujifunza.
Maelezo picha
Festo amekaa kwenye kiti anaongea na mtu wanajadiliana, chini ya miguu yake kuna kikapu cha plastiki na nyuma yake kuna vikapu vingine.
Shangazi yake Festo: Mpaka sasa hivi hata mimi la kusema nashindwa jinsi alivyofikia hapo, najua sasa hata mimi mwenyewe ananisaidia.
Maelezo picha
Festo amekaa chini anatengeneza vikapu vya plastiki, pembeni yake ni vikapu vingine vilivyokamilika taryari na nyuma yake watu wamekaa kwenye viti wakimuangalia anavyotengeneza.
Shangazi yake Festo amekaa chini ya mti anaongea. Karatasi ya mkataba wa Sense wa makubaliano ya kufanya kazi na Sense imeshikwa na mama Festo ambaye anaweka sahihi yake.
Mama yake Festo: Napenda kuwashukuru watu wa Sense kwa kumpa mwanangu muongozo huu wa kusuka vikapu kama hivi na sas hivi anajiendeleza na shughuli zake pamoja na kuwa yapo mengine madogo madogo lakini tayari wameshampa mwanga fulani na yeye anakaa tayari anajua sasa hivi nina shughuli yangu fulani.
Maelezo picha:
Mama Festo amekaa kwenye kiti akiwa ameshika karatasi na peni pembeni akiwa amezungurukwa na watu.
Mama Festo amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba akiongea.
Wanamama wamesimama na Festo huku wote wameshika vikapu vya plastiki vilivyotengenezwa na Festo.
Mama Festo amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba akiongea.
Festo: Nimekubaliana na hali yangu kama nilivyozaliwa.
Maelezo picha:
Mikono inaonekana kwa karibu ikiwa inakunja plastiki. Uso wa Festo unaonekana kwa karibu, picha mchanganyiko wa vikapu zinaonekana kutoka juu. Festo anaongea na mtu kwa lugha ya alama ambaye kwa pamoja wamekaa kwenye viti chini ya mti. Mtoto mdogo anakatisha mbele ya Festo aliyekaa chini ya mti akiwa na vikapu alivyovitengeneza.
Chapa ya Community Fund na Sense International zinatokea.