Je, hii inamfaa nani?

Walimu

Mwaka wa kuchapishwa
June 2025
Imetengenezwa na
Sense International Bangladesh

Kumuongoza mwanafunzi mwenye uziwikutoona kwenye maeneo muhimu, kuliweka darasa katika mazingira rafiki kwa ajili ya watu wenye uziwikutoona. 

Katika hali nyingi, wazazi na walimu hukutana na changamoto wanapojaribu kuwajumuisha watoto wenye Uziwikutoona katika shule za kawaida. Huenda wasijue jinsi ya kuwasaidia wanafunzi hawa darasani. Rasilimali hii itawasaidia kuelewa nini cha kufanya ili kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa Uziwikutoona kuzoea na kujifunza vizuri zaidi. 

  1. Wape wanafunzi wenye uziwikutoona mwongozo kuhusu darasa na maeneo mengine kama maktaba, choo n.k. ili wajue mahali vilipo. 
  1. Panga vifaa vyote vya darasani katika eneo maalumu. Waambie/waonyeshe kila kifaa na eneo ili waweze kuvipata kwa urahisi. 
  1. Hakikisha kuna mwangaza wa kutosha darasani na hakuna kelele zitokazo nje au ndani ya darasa. 
  1. Hakikisha wanafunzi wenye uziwikutoona wanakaa kwenye siti/eneo la mbele. Itakuwa rahisi kwa mwalimu kuwasiliana nao. Mwalimu atazungumza kwa sauti ya juu kidogo na kuandika ubaoni kwa maandishi makubwa. 
  1. Tumia vifaa vya kujifunzia na vitu halisi inapowezekana. 
  1. Fahamu njia ya mawasiliano anayoipendelea mwanafunzi (lugha ya ishara, maneno, au lugha ya mguso) na wasiliana naye kwa njia hiyo. 
  1. Waelekeze wanafunzi wengine jinsi ya kuwasaidia wenzao wenye uziwikutoona. 
  1. Panga mikutano ya mara kwa mara na wazazi wao kuhusu maendeleo ya mtoto wao. 

Pakua

Je, hii ilifaa

Maelezo haya yamekusaidia?Inahitajika
This field is for validation purposes and should be left unchanged.

Changia


Raslimali zinazofanana

Watoto wanaoishi na uziwikutoona

Shughuli za kila siku za watoto wanaoishi na uziwikutoona.

Festo – Kijana mwenye uziwikutoona, Tanzania

Video ya kijana mwenye uziwikutoona akijiingizia kipato kwa kufanya shughuli ya utengenezaji wa vikapu.

Philbert – Kijana mwenye uziwikutoona kutoka Tanzania

Ujumuishaji wa vijana wenye uziwikutoona kwenye shughuli za kiuchumi.