Je, hii inamfaa nani?
Walimu
Katika hali nyingi, mara nyingi, wazazi na walimu hukabiliwa na changamoto wanapowajumuisha watoto wenye ulemavu wa Uziwikutoona katika shule za kawaida. Huenda wasitambue namna bora ya kuwasaidia wanafunzi hawa wanapokuwa darasani. Hivyo, rasilimali hii itawasaidia kuelewa mambo gani wanapaswa kufanya ili kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa uziwi kuzoea na kujifunza vyema.
- Toa mafunzo kwa wanafunzi wenye Uziwikutoona kuhusu darasa na maeneo mengine kama vile maktaba, choo n.k. ili waweze kujua eneo lao.
- Panga vifaa vyote vya darasani katika maeneo maalum. Zitambulishe kila samani na nafasi zake ili waweze kukifkia kila kitu kwa urahisi.
- Hakikisha kwamba, darasani kuna mwanga wa kutosha na punguza kelele zinazotoka nyuma.
- Hakikisha kwamba wanafunzi wenye ulemavu wa Uziwikutoona wanakaa kwenye viti/safu ya mbele. Itakuwa ni rahisi kwa mwalimu kutangamana nao. Mwalimu atapaswa kuzungumza kwa sauti ya juu kidogo na kuandika maandishi makubwa ubaoni.
- Tumia vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na vitu vya mfano pale inapowezekana.
- Tambua njia ya mawasiliano anayoipendelea mwanafunzi (lugha ya ishara, lugha ya maneno na ya kugusa) na uwasiliane naye kwa kutumia njia hiyo
- Waonyeshe wanafunzi wengine jinsi gani wanaweza kuwasaidia wanafunzi wenzao wenye ulemavu wa Uziwikutoona.
- Andaa mikutano ya mara kwa mara na wazazi wao kuhusu maendeleo ya mtoto wao.