Je, hii inamfaa nani?
Walimu, Wazazi na walezi na maafisa wa Elimu.
Mwongozo huu, ulioandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Sense International Tanzania (E.A), unalenga kuwawezesha wasaidizi wa walimu kuwasaidia wanafunzi viziwi wasioona katika madarasa jumuishi kuanzia elimu ya awali hadi darasa la pili. Unatoa mbinu na mikakati ya kufundisha stadi mbalimbali kama kusoma, kuandika, kuhesabu, afya, mazingira, michezo na sanaa kwa kuzingatia aina ya ulemavu wa mwanafunzi na uwezo wake wa kuona na kusikia.
Mwongozo huu pia unahimiza matumizi ya mpango binafsi wa elimu (IEP), njia jumuishi za mawasiliano kama lugha ya alama na Breli, na kushirikiana na walimu, wazazi na wataalamu wengine ili kuhakikisha mazingira salama na rafiki kwa kujifunza.