Je, hii inamfaa nani?
Waalimu, Wanafunzi, Wazazi, Watunga sera na Wasimamizi
Philpert ni kijana mwenye uziwikutoona lakini hilo halimzuii kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ambazo zinamtengenezea kipato yeye na wazazi wake.
Maelekezo elekezi ya video ya Philbert
Maelezo picha:
Chapa ya Community Fund inaonekana kulia na chapa ya Sense International kushoto. Skrini inakuwa nyeusi kisha linatokea jina Philbert Mathayo mwenye uziwi na uoni hafifu kisha maandishi yanatoweka.
Maandishi yanatokea yakisomeka ‘Philbert Mathayo, kijana mwenye uziwi na uoni hafifu, anaishi mkoa wa Mwanza akijihusisha na biashara ya kuuza vinyawji na chakula kwa msaada aliopewa na wazazi wake.
Msimuliaji: Jiji la miamba kama wenyeji wanavyolipamba jiji lao, hapa ni nyumbani kwa Philbert Mathayo ulemavu wa uziwi kutoona havijamfanya kukata tamaa au kuwa tegemezi. Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe.
Maelezo picha: Bango lenye maandishi ‘karibu mkoa wa Mwanza’ linaonekana kisha sehemu ya jiji la Mwanza, mjini kamera ikizunguruka kuonyesha sehemu ya barabara za jiji la Mwanza.
Nyumba ndogo ya udongo ipo katikati ya miti huku mbele yake kukiwa na mawe mawe ya kujengea. Philbert Mathayo amekaa kwenye kiti akiongea na mtu kwa lugha ya alama.
Philbert Mathayo yupo ndani ya duka, kamera inarudi nyuma na kumuonyesha akiwa dukani. Philber anafua nguo akiwa na mama yake ambaye anamuelekeza jambo.
Mama yake Philbert: Mimi ni mzazi wa Philbert Mathayo mwenye ulemavu wa uziwikutoona, Philbert nimmzaa mwaka 1994 niligundua kama ana ulemavu ilivyofika miezi minne maana yake alikuwa akilia tu ukimuonyesha vitu kama matawi haangalii. Ndipo nilipoenda hospitali, walipomchunguza alitakiwa afanyiwe usafishaji wa macho. Kwa hiyo ndio nikawa nnimegundua kwamba kuwa mwanangu haoni.
Maelezo picha: Mama yake Philbert amesimama mbele ya nyumba huku akiongea na kutabasamu. Amekaa chini hukun anasimulia. Philbert amekaa kwenye kiti akiwa haongei jambo lolote, nyuma yake kuna mawemawe na miti.
Philbert amekaa kwenye kiti pembeni ya mama yake ambaye pia amekaa kwenye kiti huku akiendelea kusimulia.
Mtumishi wa Sense amekaa kwenye kiti na Philbert ambaye pia amekaa kwenye kiti huku wakiongea kwa lugha ya alama.
Philbert amekaa kwenye kiti pembeni ya mama yake ambaye pia amekaa kwenye kiti huku akiendelea kusimulia.
Kamera inamsogela kwa karibu Philbert ambaye amesimama wima akiwa hafanyi chochote.
Philbert amekaa kwenye kiti pembeni ya mama yake ambaye pia amekaa kwenye kiti huku akiendelea kusimulia.
Kamera inamuonyesha Philbert kwa mbali akiwa ndani ya duka lake.
Philbert amekaa kwenye kiti pembeni ya mama yake ambaye pia amekaa kwenye kiti huku akiendelea kusimulia.
Philbert anafua nguo zake mbele ya nyumba yao inayoonekana kwa mbali nyuma yake.
Mama yake Philbert: Philbert nimemlea mimi kama mimi pamoja na baba mlezi niliyekuja kumpata.
Maelezo picha:
Philbert amekaa kwenye kiti pembeni ya mama yake ambaye pia amekaa kwenye kiti huku akiendelea kusimulia.
Picha mnato ikimuonyesha Philbert akiwa amekaa na mama yake kisha inarudi kumuonyesha Philbert akiwa amekaa na mama yake anayeongea.
Baba yake Philbert: Jina langu ni Charles Kajomola, wakati nimempata mama yake, tulianza kuishi na mama yake kabla ya hapo alikuwa anaishi na bibi yake.
Maelezo picha:
Baba yake Philbert akiwa dukani dukani. Kisha anaonekana kasimama nje ya duka huku akiongea.
Bango la duka limeandikwa Mama Philbert Shop huku duka liko wazi na baba Philbert amesimama pembeni ya duka hilo.
Baba Philbert amesimama mbele ya duka huku akiongea.
Mama yake Philbert: Amemaliza shule ya msingi mwaka 2016 kwa sababu kule walikuwa wakimfundisha fani za ufundi na ujasiriamali kwa hiyo ufundi waliomfundisha ni upondaji wa kokoto. Changamoto ni nyinigi kwa mfano kwenye upande wa matibabu akiugua nilikuwa nahangaika sana kwa sababu nilikuwa sijui anaugua nini. Saa nyingine unakuta tu hivi amelala wakati mwingine analia, sasa inakuwa ugumu kwa sababu hauelewi nini kinamsumbua mpaka umpeleke hospitali, wakati mwingine vipimo vinakuwa ni vya gharama kubwa.
Maelezo picha:
Mama Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yao inayoonekana nyuma yake kwa mbali.
Philbert yupo dukani kamera ikimuonyesha kupitia nondo za mlango wa duka.
Mama Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yao inayoonekana nyuma yake kwa mbali.
Philbert amebeba nyundo ya kupasulia mawe. Kamera inamuonyesha kwa nyuma akiwa anapasua mawe.
Philbert amekaa kwenye kiti pembeni ya mama yake ambaye pia amekaa kwenye kiti huku akiendelea kusimulia.
Kamera inamuonyesha Philbert kwa karibu akiwa anapasua mawe kwa nyundo.
Philbert amekaa kwenye kiti pembeni ya mama yake ambaye pia amekaa kwenye kiti huku akiendelea kusimulia.
Mtumishi wa Sense amekaa kwenye kiti kamuelekea Philbert huku akiongea na Philbert kwa lugha ya alama.

Mama yake Philbert: Baadae nilipigiwa simu na walimu wake wakasema mwanao amepata mfadhili huku kwenye shirika moja la Sense International wakawa wametushirikisha habari za biashara wakasema tunataka kuwawezesha watoto wenu ili kusudi waweze kujikwamua kimaisha katika mahitaji yao binafsi, ndio wakasema kuwa watatuwezesha pesa kwa ajili ya kufanya biashara.
Maelezo picha:
Mama yake Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yao akisimulia.
Mama yake Philbert anatoka nje ya nyumba yake na kusogea mbele ya kamera.
Mama yake Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yao akisimulia.
Philbert amekaa kwenye kiti ametulia nyuma yake kuna mawe yaliyopasuliwa.
Mama yake Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yao akisimulia.
Wateja wanafika dukani, Philbert yupo ndani ya duka anawahudumia
Mama yake Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yao akisimulia.
Afisa biashara wilaya: Na kupitia mradi huu ambao wamefanikiwa kupewa mtaji na Sense International imeweza kusaidia hata shughuli mbalimbali za kifamilia kwa namna ambavyo wameweza kupata faida yao imewasaidia pia kusomesha wadogo zake, imewezakusaidia kupata mahitaji ya chakula, kupata mahitaji ya malazi. Kwa hiyo Sense International waendelee kuwasaidia vijana kama hawa sehemu mbalimbali Tanzania.
Maelezo picha:
Mwanadada ambaye haonekani sura ameshika jarada lenye chapa ya Sense International
Afisa biashara wilaya amesimama anaongea huku kaelekea upande wa kushoto wa kamera nyuma yake kwa mbali yanaonekana mawe.
Afisa biashara wilaya yupo nje ya duka na mama yake Philbert, huku Philbert akiwa ndani ya duka.
Watoto watatu wakifurahi kila mmoja.
Afisa biashara wilaya amesimama anaongea huku kaelekea upande wa kushoto wa kamera nyuma yake kwa mbali yanaonekana mawe.
Kamera ikionyesha nyumba ya kina Philbert huku kutoka kulia kwenda kulia
Afisa biashara wilaya yupo nje ya duka na mama yake Philbert, huku Philbert akiwa ndani ya duka.
Afisa biashara wilaya amesimama anaongea huku kaelekea upande wa kushoto wa kamera nyuma yake kwa mbali yanaonekana mawe.
Mama yake Philbert: Wakaniuliza je, unaweza kusimamia mwenye mtoto kama mtoto? Nikasema yeye hawezi. Itabidi nyinyi wazazi ndio msimamie huo mtaji.
Maelezo picha:
Mama yake Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yao inayoonekana kwa mbali.
Baba yake Philbert: Mtaji tunaulinza kwa kuhakikisha biashara yetu haishuki tunajitahidi kadri tuwezavyo kujibana ili mradi uendelee kuwepo.
Maelezo picha:
Baba yake Philbert amesimama mbele ya duka huku akiongea.
Afisa biashara wilaya: Changamoto ambazo walinielezea ni pamoja na kutokuweka vizuri kumbukumbu za mauzo na manunuzi, lakini nilijaribu kuwapa elimu wameweza kufanya hivyo. Kwa kipindi cha pili nilichokuja kuwatembelea niliona mabadiliko, wameweza kugundua sasa kwa siku wanauza shilingi ngapi na faida.
Maelezo picha:
Mama yake Philbert ameshika daftari huku akiongea na Afisa biashara wa wilaya, Philbert yupo ndani ya duka.
Afisa biashara wilaya amesimama anaongea huku kaelekea upande wa kushoto wa kamera nyuma yake kwa mbali yanaonekana mawe.
Daftari lenye mahesabu linafunuliwa huku likionyesha mahesabu ya mauzo.
Afisa biashara wilaya amesimama anaongea huku kaelekea upande wa kushoto wa kamera nyuma yake kwa mbali yanaonekana mawe.
Mama yake Philbert: Mawasiliano yangu na Philbert yapo vizuri japokuwa kuelewana kwake na yeye ni ngumu yeye anatumia alama. Mimi alama sizifahamu. Mule dukani anachowezakufanya kumuhudumia mteja labda kwa mfano mteja amekuja anataka sabuni.
Maelezo picha:
Mama yake Philbert akimuelekeza Philbert namna ya kufua kwa lugha ya alama.
Mama yake Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba.
Philbert yupo dukani, kamera inamuonyesha kupitia nondo za dukani.
Baba yake Philbert: Kwanza nashukuru Mungu, mtaji huu tulipatiwa kwa ajili yake yeye. Hata yeye mwenyewe shughuli zingine anazojishughulisha nazo kazi zake za mikono tunaweza hata kumtuma akafua nguo zetu, tunaweza hata kumtuma akafata maji kwa hiyo sio tegemezi tena kama ulivyosema ndugu mtangazaji.
Maelezo Picha:
Baba yake Philbert akiwa amesimama mbele ya duka .
Philbert anapasua mawe, kisha anamimina maji kwenye beseni.
Duka linaonekana kutoka juu na maandishi mama ‘Mama Philbert Shop’
Mama yake Philbert: Na wengine wanamthamini Philbert, mwanzoni walikuwa wakimuona mambo yake anayofanya wanasema huyu ni tahira lakini baada ya kuona shughuli zake anazozifanya wanasema yule ana akili. Kupitia watu wa Sense wameweza kusababisha mwanangu angalau ameanza kutambulika na kumuona ni mtu wakaida kabisa kama binadamu wengine waliowakamilifu.
Maelezo picha:
Mama Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yao huku akiongea.
Philbert na rafiki yake wanatembea huku wamebeba ndoo zenye maji, kamera inamuonyesha Philbert kwa nyuma akiwa amebeba ndoo mbili zenye maji.
Mama Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yao huku akiongea.
Chapa ya Sense International akionekana kwenye jarida lilishikwa na mama yake Philbert
Mama Philbert amekaa kwenye kiti mbele ya nyumba yao huku akiongea.
Mtumishi wa Sense amekaa kwenye kiti kamuelekea Philbert huku akiongea na Philbert kwa lugha ya alama.
Chapa ya Community Fund inaonekana kulia na chapa ya Sense International kushoto