Je, hii inamfaa nani?

Utambuzi na tathimini ya mapema, wazazi, waangalizi

Mwaka wa kuchapishwa
June 2025
Imetengenezwa na
Sense International Tanzania

Rasilimali hii inatoa maelezo kuhusu upimaji na utambuzi wa awali wa watoto wenye ulemavu wa uziwikutoona, ikieleza hatua za mchakato huo, huduma zinazopatikana, na jukumu la wahudumu wa afya pamoja na walezi katika kuhakikisha watoto wanaopatikana na hali hiyo wanapata msaada wa bure, wa kitabibu na kielimu unaoendana na mahitaji yao.

Sisi ni nani?

Sense International ni shirika la kimataifa linalotoa huduma kwa watu wenye ulemavu wa Uziwikutoona na wale wenye ulemavu mchanganyiko unaopelekea milango mingine ya fahamu (kuona, kusikia, kugusa na kuonja) kushindwa kufanya kazi vizuri.

Tunafanya nini?

Tunashirikiana na serikali pamoja na mashirika mbalimbali katika kuwatambua watu wenye Uziwikutoona na wale wenye ulemavu mchanganyiko ili kuwawezesha kiafya, kielimu na kujifunza stadi za maisha.

Itakuwaje kama mtoto wangu akigunduliwa kuwa na ulemavu wa Uziwikutoona?

Mtoto akigunduliwa kuwa na ulemavu wa Uziwikutoona au changamoto kwenye utendaji wa milango ya fahumu (kuona na kusikia) ataandikishwa katika kituo cha kutolea huduma ili aweze kusaidiwa na wataalamu wa tiba kwa vitendo. Wataalamu hao wataandaa utaratibu maalumu kwa kila mtoto ili kumsaidia, na kuwafundisha wazazi au walezi namna ya kusawasaidia watoto wao wakiwa nyumbani. Pia watawatembelea wanakoishi ili kujua maendeleo yao.

Tunafanyaje?

Hatua ya kwanza: Watoto wenye umri wa siku moja hadi miaka mitano watabainiwa kama wana viashiria vya kuwa na ulemavu wa uziwikutoona. Zoezi hili litafanywa na wahudumu wa afya kwa ngazi ya jamii wawapo katika vituo vya chanjo au sehemu tofauti tofauti ndani ya kata husika.

Hatua ya pili: Kama mtoto atakuwa na viashiria vya Uziwikutoona ataelekezwa kwenda kufanyiwa vipimo zaidi kwa kutumia vifaa maalumu katika moja ya vituo vifuatavyo vya afya vinavyomilikiwa na serikali, Mbagala Round Table, Yombo Vituka, Mbande, Hospitali ya Rufaa Temeke.

Ni muda gani muafaka kumpima mtoto wangu?

Kwa matokeo mazuri mtoto anatakiwa kupimwa kati ya masaa 24 baada ya kuzaliwa hadi umri wa miaka mitano.

Vipi kama mtoot wangu atakuwa na ulemavu wa aina moja tu?

Iwapo mtoto atagunduliwa kuwa na changamoto katika mlango mmoja wa fahamu (masikio au macho) ataelekezwa kuwaona wataalamu katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke watakaoweza kumsaidia kupata msaada wa kitabibu kwa utaratibu uliopo.

Je, natakiwa kulipia gharama yoyote?

Hapana, huduma hii inatolewa bure bila malipo yoyote.

Je, hii ilifaa

Changia


Raslimali zinazofanana

Mwongozo wa walezi wakati wa chakula kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuona 

Mwongozo huu unawapa walezi wa watoto wenye ulemavu wa Uziwikutoona mikakati ya vitendo, hatua kwa hatua, ya kukuza ujuzi wa kula kwa uhuru, kwa usalama, na unaochangia hisia.

Kushirikiana na Watu Wenye Ulemavu 

Rasilimali hii ni mwongozo wa vitendo unaotoa vidokezo vya adabu na mikakati ya mawasiliano kusaidia watu kuwasiliana kwa heshima na ufanisi na watu wenye aina mbalimbali za ulemavu.

Kuoga na kumvalisha mtoto mwenye uziwikutoona: Mwongozo wa hatua kwa hatua 

Huu ni mwongozo wa hatua kwa hatua unaowawezesha walezi kwa mikakati ya vitendo kusaidia watoto wenye ulemavu wa Uziwikutoona wakati wa kuoga na kuvaa, sambamba na kukuza kujitegemea, mawasiliano, na ufahamu wa mwili.