Ukurasa huu unakueleza uziwikutoona ni nini. Pia unashughulikia aina tofauti za ,uziwikutoona sababu zake kwa watoto wachanga na watu wazima, utambuzi, viashiria vya Uziwiupofu, kutibu visababisi vya msingi na kudhibiti hali hiyo.
Katika ukurasa huu utafahamu kuhusu:
- uziwikutoona ni nini?
- uziwikutoona unaathiri nini?
- Aina za uziwikutoona
- Majina mengine ya uziwikutoona
- Ni nini husababisha Uziwikutoona?
- Kubaini dalili za uziwikutoona
Uziwi kutoona ni nini?
uziwikutoonani ulemavu katika haki yake wenyewe lakini bado hautambuliwi hivyo katika nchi zote.
Inamaanisha kwamba huna uwezo wa kuona na kusikia ambao unaathiri maisha yako ya kila siku. Upatikanaji wa habari, kuwasiliana na watu na kufanya shughuli zako mwenyewe inaweza kuwa vigumu zaidi.
Kuwa na uziwikutoonahaimaanishi kwamba wewe ni kiziwi kabisa na/au kipofu kabisa. Watu wengi ambao ni Viziwivipofu wana uwezo wa kuona na wengine kusikia.
Hata ukiwa na upotevu mdogo wa kuona na kusikia, bado utapata changamoto kwa sababu ya jinsi unavyoathiriwa kwa kuwa na matatizo yote mawili ya upotevu wa kuona na ukusikia.
Shirikisho la Viziwi Dunia linafasili uziwikutoona kuwa ni muunganiko wa ulemavu ukalifu wa uoni na kusikia kiasi kwamba ni vigumu kwa hisi zilizoharibika kufidia kwa kila mmoja. Kwa hivyo, Uziwiupofu ni ulemavu tofauti. Hata hivyo ufasili wa kisheria unaweza kutofautiana kutoka nchi hadi nchi.
Nani anayeathiriwa na Uziwikutoona?
Uziwikutoona huathiri watu wa rika zote, wakiwa ni pamoja na vijana.
Ni kawaida zaidi kwa watu wazee, kwa sababu kwa asili uwezo wetu wa kuona na kusikia unakuwa mbaya zaidi kadri tunavyozeeka.
Utafiti umeonyesha kwamba asilimia 0.2 ya idadi ya watu duniani wanaishi na uziwikutoon ukalifu. Asilimia 2 zaidi ya watu ulimwenguni kote wanaishi na aina zisizo za kawaida za Uziwiupofu.*
Hii ina maana kwamba takriban watu milioni 160 wameathiriwa na . uziwikutoona
Shirikisho la uziwikutoona Dunia (2023) Ripoti ya Pili ya Dunia kuhusu Hali ya Watu Wenye wa uziwikutoona Mienendo Bora na Mapendekezo kwa ajili ya kujumuisha Watu wenye ulemavu wa uziwikutoona Machi 2023.
Aina za Uziwikutoona
Kuna aina mbili za .uziwikutoona
Uziwikutoona wa Kuzaliwa
Ulemavu wa uziwikutoona wa kuzaliwa unamaanisha kwamba umezaliwa ukiwa na ulemavu wa kuona na kusikia, au unadhihirika katika miaka miwili ya kwanza ya maisha.
Hii inaweza kuwa kwa sababu ya maambukizo wakati wa ujauzito, kuzaliwa kabla ya wakati, kiwewe cha kuzaliwa (jeraha la mwili) na hali adimu za kijenetiki (hali unazorithi kutoka kwa mzazi).
uziwikutoona Usio wa Kuzaliwa
uziwikutoona usio wa kuzaliwa humaanisha kuwa unapata upotevu wa uwezo wa kuona na kusikia baadaye maishani. Mtu yeyote anaweza kuwa na uziwikutoona wakati wowote kupitia ugonjwa, ajali au kuzeeka.
Wakati mwingine, unaweza kuzaliwa na ulemavu wa kusikia tu au uoni pekee, lakini kadri umri unavyosonga, hisi zako zingine pia huanza kubadilika au kuwa mbaya zaidi.
Majina mengine ya Uziwikutoona
Uziwikutoona pia unajuliana kama:
- Kudhoofika kwa hisia za mifumo miwili ya fahamu.
- Kudhoofika kwa hisia za mifumo mingi ya fahamu.
Watu wengi hutumia maneno haya kumaanisha maana iliyo sawa na uziwikutoona.
Wengine wanapendelea “Kudhoofika kwa hisia za mifumo miwili ya fahamu” kwa sababu wanahisi inaelezea kwa usahihi zaidi jinsi unavyojisikia kuwa uziwikutoona.
Baadhi ya watu huchagua kutumia “” uziwikutoona kuelezea kwa usahihi uoni mbaya zaidi na upotevu wa kusikia.
Kisha kuna wengine ambao wanahisi “Kudhoofika kwa hisia za mifumo mingi ya fahamu” ni sahihi zaidi.
Hii ni kwa sababu inaweza kuwa juu ya jinsi ubongo wako unavyoshughulikia habari inayopata kutoka kwenye masikio na macho yako, sio kuhusu jinsi masikio na macho yako yanavyofanya kazi. Hisia zingine, kama vile kugusa, ladha au harufu pia zinaweza kuathirika pia.
Nini kinasababisha Uziwikutoona
Kuna sababu nyingi zinazosababisha uziwikutoona wa kuzaliwa na usio wa kuzaliwa.
Visababishi vya uziwikutoonawa Kuzaliwa
uziwikutoona wa kuzaliwa unaweza kusababishwa na:
- Matatizo yanayohusiana na kuzaliwa kabla ya wakati – kuzaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito.
- Maambukizi kwa mtoto akiwa tumboni, kama vile rubella (surua ya Kijerumani), toxoplasmosis au cytomegalovirus (CMV)
- Matatizo ya kimatibabu wakati wa ujauzito na kuzaliwa – ikiwa ni pamoja na lishe duni na kiwewe
- Hali za kimaumbile, kama vile ugonjwa wa ugonjwa unaompa mtoto uwezo wa hali ya juu katika kujifunza na ugonjwa unaozuia uwezo wa mtoto kujifunza.
- Ugonjwa wa kupooza kwa ubongo – tatizo la ubongo na mfumo wa fahamu neva ambalo huathiri zaidi mizunguko na uratibu.
- Ugonjwa wa ulevi wa fetasi – matatizo ya kiafya yanayosababishwa na mama kunywa pombe wakati wa ujauzito.
Visababishi vya uziwikutoona usio wa kuzaliwa
uziwikutoonausiowa kuzaliwa unaweza kusababishwa na:
- Upotevu wa uwezo wa kusikia unaohusiana na umri.
- Dalili za Ugonjwa wa Asheri – hali ya maumbile inayoathiri kusikia, uoni na usawa.
- Matatizo ya macho yanayohusiana na umri, kama vile kuzorota kwa macula kunakohusiana na umri, mtoto wa jicho na glaukoma.
- Ugonjwa wa kudhorota kwa mishipa ya jicho kunakosabishwa na kisukari- chembechembe za nyuma ya jicho huharibiwa na viwango vya juu vya sukari kwenye damu.
- Uharibifu wa ubongo kutokana na, kwa mfano, homa ya uti wa mgongo, uvimbe wa ubongo, kiharusi au jeraha kali la kichwa.
- Malaria ya Ubongo
Kugundua Ishara za uziwikutoona
- Baadhi ya ishara za kawaida za kupoteza usikivu ni pamoja na:
- Kupata ugumu wa kusikia vizuri iwapo watu watakusemesha kwa kutokea nyuma.
- Kushtuka kwa sababu haukusikia wakati mtu akiingia sehemu uliyomo.
- Kuhitaji kuongeza sauti kwenye televisheni, redio au simu ya mkononi.
- Kuchelewa kuwajibu watu wanaozungumza nawe.
Dalili za kawaida za kupoteza uoni ni pamoja na:
- Kupata ugumu wa kuona vizuri kwenye mwanga mdogo au mwanga mkali.
- Kutokuwatambua watu unaowajua, hasa katika hali zisizotarajiwa.
- Kutegemea zaidi mguso katika kutafuta na kutambua vitu kuliko kawaida.
- Kulazimika kushikilia vitabu, magazeti au simu yako ya mkononi karibu na uso wako, au kukaa karibu na televisheni.
Ikiwa tayari una ulemavu wa kusikia/Uziwi, na pengine unavaa kifaa cha kukusaidia kusikia au kutumia lugha ya ishara, tunza macho yako. Jihadhari na dalili ya kwamba unapata pia upotevu wa kuona na utafute msaada wa kupata uchunguzi wa macho kutoka kwa Daktari wa Macho. Kwa kweli, hili inapaswa kufanywa mara kwa mara.
Ikiwa tayari una ulemavu wa kuona na labda unavaa miwani, kutumia fimbo kutembea au una hali kama vile glaukoma au mtoto wa jicho, tunza usikivu wako. Jihadhari na ishara kwamba pia unapata upotevu wa kusikia na utafute usaidizi ili kupata kipimo cha kusikia kutoka kwa Daktari ambaye ni mtaalamu wa masikio. Kwa kweli, hii pia inapaswa kufanywa mara kwa mara. Ukiona mojawapo ya ishara zilizo hapo juu, zungumza na daktari wa eneo lako au mtaalamu wa afya haraka iwezekanavyo.
Kadiri uziwikutoona unavyogunduliwa haraka, ndivyo matibabu ya haraka yanaweza kufanyika, na endapo hilo ndilo chaguo, au udhibiti wa hali unaweza kuanza na ndivyo hili linaweza kuwa ni la msaada zaidi. Hili ni muhimu hasa kwa watoto wachanga na watoto wadogo wanapokua na kukuza stadi zao za mawasiliano na hatua zingine za maendeleo.
Taarifa hii imetolewa na Sense, shirika la hisani kwa watu wenye ulemavu ambalo linaongoza kutoa misaada kwa walemavu lenye makao yake makuu nchini Uingereza ambalo linasaidia watu wenye ulemavu changamano, ikiwa ni pamoja na Uziwiupofu.
Hii imehaririwa kwa ajili ya hadhira ya kimataifa (2024).