Fungua ulimwengu wa kusoma vitabu vingi vya mtandaoni vinavyoangazia maelfu ya aina na kategoria.
Maktaba
Maktaba ni ni maktaba ya mtandaoni inayotoa mamia ya vitabu vinavyohusiana na elimu, hadithi bunifu na hadithi zisizo bunifu.
Swahili Kids
Swahili Kids inatoa vitabu anuwai vya watoto katika mada nyingi na pia inajumuisha baadhi ya rangi na laha kazi za kila kitabu.
Bloom
Bloom ina zaidi ya vitabu 250 vya Kiswahili vinavyoshughulikia vitabu vya watoto, hadithi za uwongo na za kibiblia.
Hesperian
Mwongozo wa afya wa Hesperian unatoa anuwai za nyenzo mbalimbali za afya katika Kiswahili, ikiwa ni pamoja na vitabu vya mada kama vile afya ya jamii, afya ya wanawake, na huduma ya kwanza.
Bookshare
Bookshare ina maelfu ya vitabu vinavyoweza kufikiwa katika miundo na lugha mbalimbali, vinavyokuruhusu kubinafsisha matumizi yako ya usomaji.
Maelezo ya Ufikiaji wa Tovuti
Katika baadhi ya maeneo kwenye tovuti yetu, tunashiria au kukuelekeza katika tovuti za watu wengine na programu ambazo hutoa taarifa muhimu na ushauri kwa watumiaji wetu. Hta hivyo, hatuwezi kuthibitisha kwamba tovuti na programu hizi za washirika wengine zinapatikana kikamilifu na zinatii miongozo ya WCAG 2.2.
Pale inapowezekana tunajitahidi kushirikiana na wahusika hawa kufanya mabadiliko yanayohitajika ili kuendana na miongozo ya WCAG2.2 na kuboresha ufikiaji wao.