Je, hii inamfaa nani?
• Wanafunzi
• Wazazi
• Watunga sera
Maudhui haya yanaelezea namna ya kumfundisha mwanafunzi mwenye uziwikutoona.
Manuscripti ya video
Madam Maula amekaa darasani, baadhi ya vifaa vya kufundishia kama ubao vinaonekana nyuma yake.
Madam Maula
Mahitaji ambayo mwalimu anatakiwa ayafahamu kabla hajaanza kumfundisha mtoto. Kwanza afahamu huyo mtoto ana matatizo gani kutoka na IP aliyoitengeneza. Atengeneze IP ili kujua mtoto anaweza nini? Anashindwa nini kukifanya? Anaulemavu gani?
Katuni ya mwalimu akiingia darasani huku wanafunzi wakionekana wenye furaha kumuona.
Madam Maula
Katika kuona, kusikia au ana ulemavu mwingine, pale ndio utaamua uanze unafundisha nini utaangalia na akili ilivyo. Hapo nido utaanza.
Mahitaji, yanategemea mtoto na uhitaji wake ulivyo. Kiziwi asiyeona labda kiziwi ambaye haoni kabisa hasikii kabisi lakini akili yake iko safi. Huyo tutatumia lugha alama mguso.
Katuni ya mwalimu anamsogelea mwanafunzi mwenye uziwikutoona kisha anawasiliana nae kwa lugha ya alama.
Madam Maula
Kwa sababu akili iko safi, unaweza kumfundisha kitu chochote. Unaanzia pale vitu ambavyo yeye anaweza kuvifanya, unaviboresha. Halfu ndio unaingia kwenye vitu ambavyo unataka wewe umfundishe. Kwa mfano, mtoto alikuwa anakula kwa mkono….
Wanafunzi wawili wamekaa darasani peke yao, kamera inawasogelea kwa karibu wakiwa wanakula chakula kwa kutumia vijiko.
Madam Maula
…amezoea, msadie aweze hata kutumia kijiko ili aweze kula, mtoto alikuwa anakaa chini anapokula, muweke katika kiti, muweke mezani, aweze kutumia meza kwa kula. Unakuwa unaboresha ule uelewaji wake kutoka anachoweza kwenda asichoweza. Na pia kutoka vitu vidogo vidogo kwenda vitu vikubwa. Huwezi kuanza vitu vidogo kwenda vikubwa hata elewa.
Hata vifaa vinategemea, kwa mfano kiziwi asiyeoona ambaye hana baki ya usikivu wala baki ya uoni huyu tunatumia vifaa vya kugusa zaidi. Vifaa vya kugusa zaidi inabidi mwalimu uviandae, akishagusa, utafute pia vifaa ambavyo ni halisi. Kwa hiyo atalinganisha vile vya kugusa atagusa na kifaa halisi. Kwa hiyo ataelewa alikuwa anataka nini.
Kwa mfano nataka nifundishe matunda, mtoto ajue matunda. Nitachukua chungwa nitalichora, nitaweka alama za kugusa, atagusa atajua hili ni chungwa. Halafu sasa nachukua chungwa halisi ninampa ili aelewe zaidi nitalimenya lile chungwa na kulikata na kula hapo utakuwa umemuhisha kwamba, lile nililogusa ni sawa sawa na tunda halisi, na tunda hilo likoje? Liko hivi lina utamu hivi. Kwa hiyo ukimpa kitu kingine atatofautisha chungwa na ndimu pamoja kama zinafanana kwa sababu ameshazionja umbo ni lilelile. Ukichukua ndimu kubwa na chungwa kubwa ukampa atatofautisha kwa sababu ataangalia, atagusa umbo lilivyo. Pia wakati ukilikata ataona chungwa ni tamu kuliko ndimu au limao ulilompa ashike. Kwa hiyo mtoto atakuwa ameshahuhisha maarifa kwa hiyo kumfundisha mtoto, mahitaji ya mtoto yanategemea ulemavu wake ulivyo ndio utajua mwalimu nifanye nini ili mtoto aweze kupata elimu.