Inakadiriwa kuwa watu bilioni 1.3 – kama 16% ya idadi ya watu duniani – kwa sasa wana ulemavu mkubwa
*Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu Ulemavu na Afya 2023
Karibu kwenye Kitovu cha Kimataifa cha Raslimali za ,uziwikutoona hili ni jukwaa la mtandaoni ambalo huwawezesha watu wenye ulemavu wa Uziwikutokuonauziwikutoona na wale wanaowasaidia katika upatikanaji wa maudhui, taarifa na raslimali.
Kitovu hiki kitakuwa ni ‘eneo mahsusi na la kipekee’ katika utoaji wa taarifa ambazo zinaweza kuwaongoza na kuwaelekeza watu walio na uziwikutoona na mitandao yao mipana ya usaidizi ili kuelewa na kuunganishwa kwa upana zaidi na taarifa, huduma za ndani zenye alama na mitandao.
Kwa kufanya kazi moja kwa moja na watu walio na,uziwikutoona tunataka kufika nje ya mipaka ya nchi zetu nane, tukiwasaidia kutangamana na watu wengine na ulimwengu unaowazunguka.
Kuwasaidia watu wenye uziwikutoona kuishi, kujifunza na kustawi.
Nakala ya maelezo ya uhuishaji
Msimuliaji: Watu bilioni 1.3 wenye ulemavu wanakabiliwa na hali duni ya matumizi ya kidigitali na wana uwezekano mdogo wa asilimia 35 kutokuwa na ujuzi muhimu wa kidijitali maishani mwao. Uwezo wao wa kushiriki katika jamii yetu inayoendelea kubadilika unategemea sana mazingira na teknolojia inayowezakufikiwa.
Maelezo picha: Picha ya dunia. Sehemu ya dunia inafunikwa na rangi ya njano ambayo inabadilika kuwa pembetatu, na kipande cha njano kikionyesha asilimia 35.
Maandishi ‘watu milioni 1.3’ yanaonekana kwa mtindo wa mashine ya kuandika. Picha za watu zinajitokeza chini ya pembetatu.
Kamera inashuka chini ili kuonyesha vifaa vitatu vya kidijitali, vikiwemo simu, kishikwambi, na kompyuta mpakato.
Msimuliaji: Ni mtoto mmoja tu kati ya watoto watano wenye Uziwikutoona ambaye ameandikishwa katika shule ya msingi, na ana uwezekano mdogo wa kuajiriwa mara kumi zaidi kuliko wenzao wasiokuwa na Uziwikutoona.
Maelezo picha: Picha za watoto wakikimbia zikiwa zimezungushiwa mwangaza wa njano. Wanakimbia wakipita majengo hadi kwenye eneo jeupe tupu. Kamera inahama, inamuonyesha kijana mmoja, akiwa na mwangaza wa njano, kwenye maeneo ya jiji.
Msimuliaji: Kitovu cha Kimataifa cha Rasilimali za Uziwikutoona kinalenga kubadilisha hali hii kwa kutoa maudhui yanayopatikana, nyenzo, na taarifa kwa lugha 7, kuwaunganisha na kuwawezesha watu wenye Uziwikutoona pamoja na wahisani wao.
Maelezo picha: Kamera inasogea na maandishi ya ‘Kitovu cha Uziwikutoona Duniani’ yanaonekana kwa mtindo wa mashine ya kuandika. Vifaa mbalimbali vya kidijitali vinaonekana – picha kama kompyuta na kompyuta mpakato. Alama za kidijitali zinatoweka na neno “Rasilimali” linaonekana katika lugha saba tofauti kuzunguka maandishi hayo.
Msimulizi: Kutana na Alice kutoka Tanzania. Alice ni msichana mwenye umri wa miaka tisa na asiyeweza kuona vizuri na asiyeweza kusikia.
Maelezo picha: Alice anaonekana akiwa na mwangaza wa rangi ya samawati.
Msimuliaji: Anaishi vijijini Tanzania na familia yake na ana ndugu wengi wanaomsaidia katika shughuli zake za kila siku na michezo.
Maelezo picha: Alice anasogea upande wa kulia na picha ya watoto wadogo walioinua mikono yao wakiwa wamekaa kwenye madawati yao darasani inaonekana upande wa kushoto. Watoto watano waliovaa sare za shule wanakimbia kutoka shuleni, wakiwa na mwangaza wa njano. Alice bado yuko upande wa kulia.
Msimulizi: Kwa miaka mingi, Alice hakuweza kuhudhuria shule, jambo lililochelewesha maendeleo ya ukuaji wake kijamii na kiakili. Ulimwengu wake ulijumuisha mazingira yake ya karibu pekee.
Maelezo picha: Kamera inasogea kwa haraka kuonyesha shule iliyo karibu na nyumbani kwa Alice. Watoto wengine wanakimbilia kushoto kuelekea shuleni. Kamera inasogea kwa Alice, aliyebaki nyumbani peke yake.
Msimuliaji: Hali hiyo iliendelea hivyo hadi pale Sense International ilipohusishwa.
Maelezo picha: Alice na nyumba yake polepole wanatoweka na maandishi ya ‘Sense International’ yanaonekana.
Msimuliaji: Sense International ilimtambulisha mama yake Alice kwenye Kitovu cha kimataifa cha Rasilimali za Uziwikutoona.
Maelezo picha: Maandishi yanatoweka na kamera inasogea kwenye picha ya wanawake wawili wa Kiafrika ambao ni mwalimu na mama yake Alice. Mama Alice anashikilia kishikwambi. Vifaa vya kidijitali, kompyuta mpakato, kishikwambi, na simu ya mkononi vinaonekana juu ya wanawake hao wawili, zinazoonyesha Kitovu cha Rasilimali za watu wenye Uziwikutoona.
Msimuliaji: Alionyeshwa video maalumu za mafunzo, zilizompatia mwongozo na shughuli za kusisimua hisia kwa Alice.
Maelezo picha: Kishikwambi kinainuka kutoka nafasi ya kulala na kuwa wima na kuonyesha skrini za Kitovu cha kimataifa cha Rasilimali za watu wenye uziwikutoona. Alama zinaonyesha ‘miongozo’, ‘uchocheaji wa hisia’, na ‘shughuli’ vinaonekana.
Msimuliaji: Alice ameendelea kustawi tangu wakati huo na anahudhuria shule mara kwa mara, akitumia Kitovu hicho pamoja na mwalimu wake maalumu. Pia anashiriki katika shughuli za jamii na ana marafiki.
Maelezo picha: Mistari yenye vidoti inatoka kwenye kishikwambi, ikielekea kwa madirisha tofauti. La kwanza linaonyesha Alice na mwalimu wake, pamoja na fremu inayoonyesha matumizi kwenye Kitovu. Kuna video kutoka Kitovu, na maneno “zana za darasani” na “teknolojia saidizi” yanajitokeza kwenye viputo vya rangi ya bluu. Kamera inarudi nyuma na kuhama hadi kwenye dirisha linalofuata, ikisogea kuonyesha mama yake Alice akishikilia kishikwambi, ikiwa na fremu inayoonyesha matumizi ya Kitovu. Maneno “Miongozo ya Wazazi”, “Vidokezo vya ustawi” na “Vitabu” yanaonekana kwenye viputo vya samawati kuzunguka skrini. Kamera inarudi nyuma na kusogea haraka hadi kwenye picha inayoonyesha Alice na rafiki yake wakisoma pamoja, na inahama hadi kwenye picha ya kundi la watoto waliokaa wakitazama kishikwambi kilichoshikiliwa na msichana mdogo.
Msimuliaji: Kitovu cha kimataifa cha Rasilimali za Uziwikutoona kinaweza kuwa dirisha la kuelekea ulimwenguni kwa watu wazima na watoto wengi, kama ilivyokuwa kwa Alice.
Maelezo picha: Picha zinatoweka moja baada ya nyingine, na kubakisha maandishi ‘Kitovu’ na kishikwambi kisichokuwa na maandishi. Kamera inasogea kwenye kishikwambi, ambapo Picha ya Dunia inaonekana ikiwa na miale ya samawati inayotoka nje yake.
Msimuliaji: Kwa pamoja, tunaweza kujenga nafasi na rasilimali zinazowezakufikiwa, ili kuhakikisha kila mtu, kama Alice, anajumuishwa na kuunganishwa.
Maelezo picha: Picha ya Dunia inatoweka na kwenye mandhari nyuma nyeupe, nembo ya Sense International inaonekana. Maneno “Ungana. Jifunze. Shiriki” yanaonekana haraka pamoja na tovuti ya kitovu cha rasilimali za watu wenye uziwikutoona. Hatimaye, nembo ya ‘Kitovu cha Uziwikutoona Duniani’ na chapa ya ‘Nelumbo Stiftung’ zinaonekana katikati chini ya skrini
Saidia kuanza
Uziwikutoona ni nini
Ukurasa huu unakueleza uziwikutoona ni nini. Pia unashughulikia aina tofauti za ,uziwikutoona sababu zake kwa watoto wachanga na watu wazima, utambuzi, viashiria vya Uziwiupofu, kutibu visababisi vya msingi na kudhibiti hali hiyo.
Jinsi ya kumsaidia mtoto mwenye uziwikutoona katika miaka yake ya awali
Miaka ya awali ya maisha ya mtoto inaweza kuwa mkondo wa kujifunza kwa wazazi. Katika ukurasa huu utaweza kutapata majibu ya baadhi ya maswali ya kawaida zaidi ambayo huulizwa na wazazi na walezi wa watoto wadogo wenye ulemavu changamano.
Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu
Huu ni uwasilishaji mfupi wa baadhi ya haki za watu wenye ulemavu, kama zinavyofafanuliwa katika vifungu vya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu. Hii sio hati ya kisheria.
Njia za kuwasiliana na mtu mwenye uziwikutoona
Kuna maelfu ya njia za kuwasiliana na kuunganishwa – iwe kwa hotuba, lugha ya alama, mguso, harakati, ishara, sauti, picha, vitu au vifaa vya kielektroniki.Kumbuka, bado hujachelewa kuanza kujifunza njia mpya ya kuwasiliana. Nenda na usijali kuhusu kukosea.
Raslimali kwa ajili ya kufundishia, malezi, kujifunzia na kustawi
- Maisha na kujifunza
- Habari
- Vitabu
- Mtaalamu na Kiufundi
- Program tumizi za simu
- Teknolojia ya usaidizi
- Kuuelewa Uziwikutoona
- Msaada wa ndani
Upendo wa Dipak wa kujifunza

“Dipak anastahili kupata mazingira sawa ya kujifunza kama ilivyo kwa mtu mwingine, na kumwezesha kuendelea kustawi.”
Mwalimu wa Dipak